Pata taarifa kuu
DRC-MAREKANi-UFARANSA-SIASA-USALAMA

Marekani na Ufaransa wakaribisha hatua ya Joseph Kabila

Saa chache baada ya kutangazwa mgombea urais atakayepeperusha bendera ya chama tawala DRC, PPRD, na washirika wake, Marekani na Ufaransa wamekaribisha hatua ya rais Joseph kabila ya kutowania katika Uchaguzi Mkuu wa Desemba 23.

Emmanuel Ramazani Shadary anawasalimu wafuasi wake wakati akiwasili kwenye makao makuu ya Tume ya Uchaguzi huko Kinshasa, Agosti 7 kuwasilisha rasmi fomu yake ya kuwania katika uchaguzi wa urais wa Desemba 23.
Emmanuel Ramazani Shadary anawasalimu wafuasi wake wakati akiwasili kwenye makao makuu ya Tume ya Uchaguzi huko Kinshasa, Agosti 7 kuwasilisha rasmi fomu yake ya kuwania katika uchaguzi wa urais wa Desemba 23. © REUTERS/Kenny Katombe
Matangazo ya kibiashara

Marekani imebaini kwamba hatua ya Kabila itaruhusu mckatao wa kidemokrasia unaendelea kusonga mbele nchini DRC.

"Tunakaribisha taarifa kwamba rais Kabila hatawania muhula wa tatu kulingana na Katiba ya nchi yake," balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Nikki Haley amesema katika taarifa.

Waziri wa zamani wa usalama nchini DRC Emmanuel Ramazani Shadary ndiye atakayepeperusha bendera ya chama tawala wakati wa Uchaguzi wa urais mwezi Desemba.

Hatua hii imekuja baada ya kuteuliwa hapo jana na rais Joseph Kabila, ambaye ni rasmi kuwa hatawania.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.