Kongamano la wadau wa mawasiliano Afrika, kufanyika Tanzania Mei 25
Kongamano la wadau wa mawasiliano Afrika linatarajiwa kufanyika nchini Tanzania siku ya Ijumaa ya Mei 25 mwaka huu ambapo litawakutanisha wadau wa uhusiano na mawasiliano kutoka taasisi mbalimbali za ndani na nje ya Tanzania.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Kongamano hilo litafanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Ofisi ndogo ya Bunge la Tanzania iliyopo Dar es salaam kuanzia saa nne asubuhi hadi saa nane mchana.
Kongamano hilo lenye kichwa cha “Uchumi wa pamoja Afrika:Machango wa mawasiliano katika kuchochea ufanisi wa sera ya viwanda Tanzania na Afrika kwa ujumla”
Rais wa chama cha maofisa Uhusiano Tanzania, Loth Makuza ameiambia RFI Kiswahili kuwa kongamano hilo linafanyika ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya mawasiliano Afrika.
“Tukio hili linalenga wanataaluma katika nchi za Afrika kukutana na kujadili masuala mbalimbali na kutathimini mchango wa mawasiliano katika bara la Afrika,”.
Ripoti zaidi zinasema kwa mwaka huu, wiki ya mawasiliano inatazamiwa kuadhimishwa katika miji mikubwa 60 iliyopo Afrika, Asia na Ulaya.