RSF: Uhuru wa habari upo mashakani
Shirika la Kimataifa linalotetea wanahabari linasema, uhuru wa wahabari upo mashakani sana kote duniani, wakati ambapo wanahabari wengi wametoweka, na wengine wanafungwa katika nchi mbalimbali duniani.
Imechapishwa:
Reporters Without Borders, linasema wanahabari katika mataifa mbalimbali wanateswa, wanafungwa jela na hata kupotea katika mazingira yasiyoeleweka.
Barani Afrika baadhi ya mataifa yanayoelezwa kuongoza katika unyanyasaji wa wanahabari na uhuru wa kufanya kazi zao ni pamoja na DRC, Congo, Djibouti, Eritrea na Zimbabwe.
Hayo yanajiri wakati ambapo mapema wiki hii Mahakama ya kijeshi nchini Cameroon ilimhukumu kifungo cha maisha jela mwandishi wa habari wa Idhaa ya Hausa ya RFI nchini humo kwa kosa la kutetea ugaidi.
Hata hivyo uongozi wa RFI ulisema kuwa Ahmed Abba hana hatia yoyote, ukibaini kwamba alifanya kazi yake kulingana na sheria.
Uongozi wa RFI unaendelea kuomba Ahmed Abba achiwe huru mara moja.