Pata taarifa kuu
ICC

Bemba apewa kifungo cha mwaka mmoja kwa kuwahonga Mashahidi

Makamu wa rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jean-Pierre Bemba amehukumiwa jela mwaka mmoja na Mahakama ya Kimataifa ya ICC na kutakiwa kulipa faini ya Euro 300,000 baada ya kupatikana na kosa la kuwahonga mashahidi.

Jean-Pierre Bemba (Kulia) akiwa katika Mahakama ya ICC
Jean-Pierre Bemba (Kulia) akiwa katika Mahakama ya ICC REUTERS/Michael Kooren
Matangazo ya kibiashara

Adhabu hii imeongezwa katika hukumu ya awali aliyopewa ya miaka 18 jela mwaka 2016, baada ya kupatikana na kosa la kuhusika na uhalifu wa kivita kwa kutuma jeshi lake kwenda nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, kati ya mwaka 2002 na 2003 na kuhusika na visa mbalimbali vya ukiukwaji wa haki za binadamu.

Majaji wametoa hukumu hii baada ya kufunguliwa mashtaka hayo, akishirikiana na watu wengine wanne kwa kuwahonga mashahidi ili kutoa ushahidi wa uongo kuhusu kesi yake.

Majaji katika Mahakama hiyo wamebaini kuwa Bemba alitumia simu na lugha za siri kuwahonga mashahidi hao.

“Mahakama hii inakupa kifungo cha miezi mingine 12 na kitakwenda sambamba na kifungo cha awali cha miaka 18,” Jaji Bertram Schmitt amemwambia Bemba.

Mahakama hiyo imesema hukumu hii itatoa funzo kwa na imetuma ujumbe kwa wale wote wanaozuia upatikanaji na haki katika Mahakama hiyo.

Hii imekuwa ni kesi ya kwanza, kuhusu kuhongwa kwa mashahidi na kutolewa uamuzi na Mahakama hiyo yenye makao yake mjini Hague nchini Uholanzi.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.