Pata taarifa kuu
LIBYA-WAHAMIAJI

Wahamiaji 6,500 waokolewa katika pwani ya Libya

Maafisa wa uokoaji wa majini wa Italia, ambao waliratibu Jumatatu zoezi la kuwaokoa wahamiaji 6,500 katika pwani ya Libya, hofu mpya ya kuongezeka kwa rekodi inatazamiwa Jumanne hii katika eneo la Mediterranean.

Wahamiaji ambao wamekua wakijaribu kuingia Ulaya wakipitia katika bahari ya Mediterranean, wengi wamepoteza maisha.
Wahamiaji ambao wamekua wakijaribu kuingia Ulaya wakipitia katika bahari ya Mediterranean, wengi wamepoteza maisha. AFP PHOTO / ALBERTO PIZZOLI
Matangazo ya kibiashara

"Tumekuwa hasa na kazi kubwa leo," msemaji wa kikosi cha waokoaji wa majini wa Italia ameliambia shirika la habari la AFP. Awali maafisa wa uokoaji wa Italia walikataa kwa siku nzima ya Jumatatu hii kuzungumzia kuhusu rekodi iyo mpya.

Lakini Kwa mujibu wa afisa huyo, hali ya hewa itachangia kwa kuongezeka kwa idadi mpya ya matukio kama hayo Jumanne hii.

Safari ya wahamiaji kutoka Libya zimekua zikikumbwa na mfululizo wa mawimbi, pamoja na kuongezeka kwa shughuli za uokozi wakati kuna kuwa utulivu wa maji baharini.

Watu wengi wamepoteza maisha yao katika safari kama hizi, baadhi wamekua wakitokea katika vita zilizokumbwa na vita na wenginea wamekua wakijaribu kuvuka bahari kwa minajili ya kwenda kutafuta maisha borabarani Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.