Pata taarifa kuu
IAAF-RIADHA

Riadha: Kamati ya kimataifa ya Olimpiki yamsimamisha kwa muda Lamine Diack

Shirikisho la kimataifa la Olimpiki limeamua, Jumanne wiki hii, kumsimamisha kwa muda Lamine Diack, mjumbe wa heshima wa taasisi hiyo na rais wa zamani wa Shirikisho la Kimataifa la Riadha (IAAF), aliyefanyiwa uchunguzi wa tuhuma za kashfa ya rushwa na kujitajirisha kwa kiasi kikubwa.

Lamine Diack, rais anayemaliza muda wake wa IAAF, katika mkutano na waandishi wa habari mjini Beijing, Agosti 21, 2015.
Lamine Diack, rais anayemaliza muda wake wa IAAF, katika mkutano na waandishi wa habari mjini Beijing, Agosti 21, 2015. AFP/AFP/Archives
Matangazo ya kibiashara

"Kamati tendaji ya Shirikisho la kimataifa la Olimpiki imeamua Jumanne hii mchana kufuata pendekezo la kamati ya maadili kwa kumsimamisha kwa muda Lamine Diack", Shirikisho la kimataifa la Olimpiki limesema katika taarifa yake.

Lamine Diack, raia wa senegali, mwenye umri wa miaka 82 na Rais wa Shirika la kimataifa la Riadha (IAAF) kwa kipindi cha miaka 15 hadi mwezi Agosti mwaka jana, alifanyiwa uchunguzi wa tuhuma za kashfa za rushwa iliyokithiri na kujitajirisha kwa kiasi kikubwa katika kesi ya matumizi ya dawa za kuongeza nguvu mwilini nchi Urusi.

Jumatatu wiki hii, Shirikisho la kimataifa la Olimpiki liliamua kuwasilisha tuhuma hizo mbele ya kamati yayake ya maadili kuhusu.

Mshauri wake wa masuala ya kisheria, wakili Habib Cissé, mwenye umri wa miaka 44, alichunguzwa pia, kwa tuhuma za kashfa ya rushwa pekee, pamoja na daktari Mfaransa Gabriel Dollé, ambaye alikuwa msimamizi wa kitengo kinacho pambana dhidi ya dawa za kuongeza nguvu mwilini katika Shirikisho la kimataifa la Riadha hadi mwisho wa 2014.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.