Pata taarifa kuu
WADA-URUSI-IAAF-RIADHA

Wada yataka Urusi isimamishwe katika mashindano ya Kimataifa ya riadha

Shirika linalopambana na matumizi ya dawa za kusisimua au kuongeza nguvu mwilini kwa wanamichezo duniani Wada, limependekeza kuwa Urusi ifungiwe kushiriki katika mashindano ya Kimataifa ya riadha.

Mariya Savinova, Mrusi katika fainali ya mita 800 katika mashindano ya kimataifa ya riadha.
Mariya Savinova, Mrusi katika fainali ya mita 800 katika mashindano ya kimataifa ya riadha. AFP PHOTO / KIRILL KUDRYAVTSEV
Matangazo ya kibiashara

Hii ni baada ya Kamati ya wachunguzi kutoka Shirika hilo kusema kuwa wanariadha wamekuwa wakitumia dawa za kusisimua misuli katika mashindano mbalimbali na pia wamekuwa wakilindwa na maafisa wa Shirikisho la raidha duniani IAAF.

Hata hivyo polisi ya kimataifa (Interpol) itaratibu uchunguziwa kimataifa wa kashfa hiyo.

Kamati hiyo pia inataka wanariadha watano na makocha watano kufungiwa maisha kushiriki katika maswala ya riadha.

Mapendekezo haya yanatolewa wakati huu rais wa zamani wa Shirikisho la riadha duniani IAAF Lamine Diack, raia wa Senegal, akichunguzwa na Polisi wa Ufaransa kwa tuhma za kupokea fedha ili kuwapa adhabu wanariadha wanaotumia dawa za kusisimua misuli tuhma ambazo amezikanusha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.