Pata taarifa kuu
URUSI-IAAF-WADA-RIADHA

Riadha: Urusi yajitetea, kashfa yatishia kusambaa

Jumanne wiki hii, Urusi imefutilia mbali madai ya matumizi ya dawa za kusisimua au kuongeza nguvu mwilini pamoja na kashfa ya rushwa ambavyo vinaikabili, na kuahidi majibu ya haraka ili kuepuka kupigwa marufuku katika michezo ya Olimpiki-2016.

Rais wa Urusi Vladimir Putin (kushoto) na msemaji wa Kremlin, Dmitry Peskov Kremlin, Oktoba 6 katika mji wa Astana.
Rais wa Urusi Vladimir Putin (kushoto) na msemaji wa Kremlin, Dmitry Peskov Kremlin, Oktoba 6 katika mji wa Astana. Sergei Guneev/RIA NOVOSTI/AFP/Archives
Matangazo ya kibiashara

Urusi imesema kashfa hiyo ni kubwa na inatishia kuenea katika nchi nyingine na michezo mingine.

" Madai haya hayana msingi ", msemaji wa Kremlin, Dmitry Peskov amesema wakati wa mkutano na waandishi wa habari, akiamini kwamba tuhuma hizo "hazina ushahidi".

Kwa upande wake, Shirikisho la Riadha nchini Urusi limesema "hivi karibuni litawasilisha kwa Shirikisho la kimataifa la Riadha IAAF hati kwenye programu yake ya kupambana na dawa za kuongeza nguvu mwilini, na hatua madhubuti katika utekelezaji wake ", Shirikisho la Riadha nchini Urusi limehakikisha katika taarifa yake, huku ikisema kuwa "ushirikiano hakika (na IAAF) utakuwa wenye ufanisi zaidi kuliko uamzi wowote wa kusimamishwa au kutengwa."

Kwa mujibu wa Urusi ya Vladimir Putin, ambayo iliandaa michezo ya Olimpiki ya majira ya joto katika mji wa Sochi mwaka 2014 na itakuwa mwenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018, muda ni mfupi: ina muda hadi mwishoni mwa wiki hii ili kujibu tuhuma ziliotolewa katika ripoti ya Jumatatu wiki hii na Shirika la kimataifa linalopinga matumizi ya dawa ya kusisimua mwili (Wada), ambalo linaituhumu "matumizi ya dawa zakusisimua mwili yaliopangwa" kuanzia kwa wanariadha wake hadi kwenye uongozi wa juu serikalini. Vinginevyo kuna hatari ya kusimamishwa katika mashindano ya riadha, ikiwa ni pamoja na Michezo ya Olimpiki-2016 katika mji wa Rio.

Mbali na kesi ya Urusi, swali gumu laulizwa: Kashafa hii itaendelea kuzikumba nchi nyingine na michezo mingine? Kama jibu ni ndio, uaminifu wa michezo na maadili ambayo yanatakiwa kuletwa yatapata pigo kubwa, ikiwa imesalia miezi tisa ya Michezo ya Olimpiki ya Rio, na miezi saba ya michuano ya Kombe la mataifa ya Ulaya nchini Ufaransa. Hayo yanajiri wakati ambapo Shirikisho la Soka Duniani FIFA linakabiliwa na kashafa ya rushwa tangu miezi kadhaa iliyopita.

Wakati huo huo Kenya, taifa la pili ambalo liko hatarini kufuatia tuchunguzi wa hivi karibuni, haikua na wasiwasi na tuhuma hizi za shirika la kimataifa linalopinga matumizi ya dawa za kusisimua mwili (Wada). Lakini matumizi ya dawa za kusisimua mwili na rushwa yameendelea kuenea, na kutia wasiwasi katika nchi hii ya Afrika Mashariki, kwa mujibu wa wataalamu.

Wakati wa mashindano ya Marathon, Nairobi , Oktoba 25, 2015.
Wakati wa mashindano ya Marathon, Nairobi , Oktoba 25, 2015. REUTERS/Noor Khamis

"Kama Wakenya hawapati matokeo kuhusu [matumizi ya dawa za kusisimua mwili], mtu mwingine atfanya kazi kwenye nafasi yao",Dick Pound, rais wa zamani wa Shirika la kimataifa linalopinga matumizi ya dawa za kusisimua mwili (Wada), ameonya Novemba 9, 2015.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.