Pata taarifa kuu
RIADHA

Wanariadha kutoka Kenya waibuka mabingwa mbio za Berlin Marathon

Wakenya wamenyakua nafasi ya kwanza katika mashindano ya riadha ya Berlin Marathon mwaka huu yaliyofanyika Jumapili hii nchini Ujerumani.

Eliud Kipchoge bingwa wa Berlin Marathon 2015
Eliud Kipchoge bingwa wa Berlin Marathon 2015
Matangazo ya kibiashara

Kwa upande wa wanaume, Eliud Kipchoge aliibuka wa kwanza lakini akashindwa kuvunja rekodi ya mbio hizo baada ya kumaliza kwa muda wa saa 2, dakika 04 nukta 01.

Kipchoge alikuwa analenga kuvunja rekodi ya Mkenya mwenzake Dennis Kimetto aliyeweka rekodi ya saa 2 dakika 2 na sekunde 57 aliyoiweka mwaka uliopita.

Kipchoge amesema licha ya kushindwa kuvunja rekodi ya Kimetto, amefurahi sana kuibuka mshindi mwaka huu licha ya kiatu chake kumsumbua.

“Nafurahi sana kuweka rekodi nzuri ya binafsi, licha ya kutaka kuvunja rekodi,” alisisitiza.

Nafasi ya pili ilichukuliwa na Mkenya mwingine Eliud Kiptanui na Feyisa Lilesa kutoka Ethiopia akimaliza ya tatu.

Gladys Cherono mshindi mwaka 2015 Berlin Marathon
Gladys Cherono mshindi mwaka 2015 Berlin Marathon

Kwa upande wa wanawake, Gladys Cherono pia kutoka nchini Kenya alimaliza wa kwanza kwa muda wa saa 2 dakika 19 na sekunde 25.

Cherono mwenye umri wa miaka 32 amesema amefurahi sana kushinda mbio hizi na anatumai kuwa ataendelea kukimbia kwa kasi katika siku zijazo.

Mwaka 2012, Cherono alikuwa mwanariadha wa kwanza barani Afrika kushinda mbio za Mita 5000 ma 10000 wakati wa mashidano ya bara Afrika.

Nafasi ya pili katika mbio hizi za Berlin Marathon mwaka huu ilichukuliwa na Aberu Kebede kutoka Ethiopia na Maseret Haili pia kutoka Ethiopia akimaliza wa tatu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.