Pata taarifa kuu
UMOJA WA AFRIKA-MKUTANO-BURUNDI

AU yatoa baadhi ya matumaini kwa upinzani

Maazimio ya Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika kuhusu Burundi hatimaye yametolewa Jumapili mwishoni mwa juma hili lililopita mjini Johannesburg nchini Afrika Kusini. Mkutano huo uliyowashirikisha marais kutoka bara la Afrika uliofanyika Jumamosi jioni.

Wapinzani dhidi ya muhula wa tatu wa rais Pierre Nkurunziza wakiandamana Bujumbura, Juni 4 mwaka 2015.
Wapinzani dhidi ya muhula wa tatu wa rais Pierre Nkurunziza wakiandamana Bujumbura, Juni 4 mwaka 2015. REUTERS/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Iwapo upande wa serikali ya Burundi, wameridhishwa na ziara ya mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, wapinzani kadhaa kwa upande wao wanaona katika maamuzi yaliyotolewa na baraza la amani na usalama la Umoja wa Afrika sababu ya matumaini, hata kama suala la awamu ya tatu limewekwa kando.

Mambo muhimu katika maazimio hayo yanapatikana katika Ibara ya 10 ya tangazo la Baraza la Amani na Usalama. Maamuzi sita yanatoa mwelekeo wa jinsi mambo yanavyopaswakwenda nchini Burundi. Jambo la kwanza ni kuanza kwa mazungumzo kati ya serikali ya Burundi na upinzani ndani ya wiki moja baada ya tangazo la baraza la Amani na Usalama, yaani Jumamosi ijayo.

Timu itakayosimamia mazungumzo itaundwa baada ya mazungumzo yatakayoendeshwa na uongozi wa Tume ya Umoja wa Afrika, chni ya mwamvuli wa rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete, mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Lengo la mjadala huu ni kujenga mazingira mazuri kwa ajili ya uchaguzi, lakini pia kutatua masuala yote yanayosababisha mgongano kati ya pande husika nchini Burundi.

Uamzi wa tatu unahusu uchaguzi: kalenda iliyotangazwa na serikali, haitazingatiwa. Tarehe ya uchaguzi itawekwa kwa makubaliano ya pande zote husika katika mchakato wa uchaguzi kulingana na uamzi uliyochukuliwa na jumuiya ya Afrika Mashariki wa kuahirisha uchaguzi kwa kipindi cha mwezi mmoja na nusu.

Baraza la amani na usalama pia limetangaza kutumwa aina tatu ya timu zake za wajumbe nchini Burundi. Timu ya kwanza itaundwa na waangalizi wa haki za binadamu, timu ya pili itajihusisha na kuchunguza mchakato wa kuwapokonya silaha wanamgambo, ambayo itaundwa na wataalam na wanajeshi. Na timu ya tatu itajielekeza Burundi kama masharti yatakua yameheshimishwa kwa ajili ya uchaguzi usiyokuwa na kasoro. Timu hii ni ya ujumbe wa waangakizi wa uchaguzi ambao utapelekea Umoja wa Afrika kuamua au la kutambua matokeo ya uchaguzi.

Na kuhakikisha utekelezaji wa maamuzi haya, ujumbe wa mawaziri kwa ushirikiano wa Tume ya Umoja wa Afrika utajielekeza wiki ya kwanza ya mwezi Julai nchini Burundi.

Ujumbe wa Afrika Mashariki mjini Bujumbura

Wakati huo huo, kama ilivyoahidiwa, ujumbe wa mawaziri wa mambo ya nje wa kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wamewasili mjini Bujumbura kwa ziara ya kutathmini utekelezaji wa maazimio yaliyopitishwa na mkutano wa kilele wa Dar es Salaam mwishoni mwa mwezi Mei. Mawaziri wawili wa mambo ya nje, mmoja kutoka Tanzania na na mwengine kutoka Uganda, wamewasili mjini Bujumbura Jumapili usiku juni 14, kwa mujibu wa vyanzo kidiplomasia. Lakini hakuna taarifa iliyeweza kuthibitishwa kama mawaziri wa mambo ya nje wa Rwanda na Kenya, ambao bado wako nchini Afrika Kusini, watajiunga na wenzao baadaye, licha ya kuwa wizara ya mambo ya nje ya Burundi ilikataa kutoa taarifa yoyote kuhusu ziara hiyo.

Katika ajenda ya ujumbe wa jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki, mawaziri hao wanatazamia kukutana kwa mazungumzo na rais Pierre Nkurunziza bila shaka. Lakini leo Jumatatu asubuhi, watakuwa na mkutano wa kwanza na viongozi wa vyama vya kisisa vya upinzani vinaopinga muhula wa tatu wa Pierre Nkurunziza.

“ Unaona kuwa Serikali imekataa mazungumzo yaliyopendekezwa katika mkutano wa kilele wa Dar es Salaam. serikali pia imepuuza masuala yote yaliyopendekezwa katika mkutano wa kilele mjini Dar es Salaam, na mawaziri wanarurudi kuzikiliza pande zote husika katika mchakato wa uchaguzi ili waweze kutoa tena ripoti kwa marais wa Ukanda huu ambao watakutana haraka kuamua hivi sasa kuchukua hatua za kisheria hatua dhidi ya rais Nkurunziza, kwa kumueleza kwamba hapaswi kulazimisha uchaguzi huu", amesema msemaji wa upinzani, Jérémie Minani.

Alain Aimé Nyamitwe, waziri wa mambo ya nje wa Burundi amesema hana wasi wasi : " Sina hofu kwa sababu jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki ni jumuiya yetu. Siwezi kueleza lolote juu ya nini watazungumzia, lakini kilicho muhimu zaidi ni kwamba serikali bado iko tayari kuwasikiliza, kufanya kazi pamoja nao ".

Akiulizwa kuhusu iwapo anahofu kuwa ujumbe huo utaomba uchaguzi uahirishwe kwa mara nyingine tena, Alain Aimé Nyamitwe amesema si lazima.

" Sina hofu. Katika hali yoyote, ninacho jua mimi ni kwamba chochote kitachotokea, mapendekezo yoyote yatayotolewa na mawaziri hawa lazima yaidhinishwe na marais", amesema Nyamitwe waziri wa mambo ya nje wa Burundi.

Marais wa jumuiya ya Afrika Mashariki wanatazamia kukutana ndani ya majuma mawili, yaani baaada ya uchaguzi uliyopangwa na utawala peke yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.