Pata taarifa kuu
BURUNDI - DIPLOMASIA

Baraza la usalama la AU lakutana kujadili kuhusu mzozo wa Burundi

Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika linakutana tangu leo Jumamosi jijini Johanesbourg, ikiwa ni siku moja kabla ya mkutano wa viongozi wa Umoja wa Afrika hapo kesho, kujadili kuhusu mzozo wa Burundi pamoja na kuongezeka kwa makundi ya kigaidi katika bara la Afrika lakini pia mzozo wa Sudani Kusini.

Machafuko ya kisasa nchini Burundi
Machafuko ya kisasa nchini Burundi reuters
Matangazo ya kibiashara

Ikiwa ni majuma mawili kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa wabunge na wamadiwani wakati ambapo juhudi za kidiplomasia kuutafutia suluhu ya mzozo wa kisiasa zikionekana kugonga mwamba wakati huu serikali ikitupilia mbali uwezekano wa kurefusha tena muda wa uchaguzi huo au kujadili kuhusu muhula wa 3 wa rais Pierre Nkurunziza.

Wakati huo huo, upinzani nchini Burundi unaopinga nia ya rais wa Burundi Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu tangu April mwaka huu, umelaani vikali hatuwa ya serikali kuendelea kutumia nguvu katika mchakato wa uchaguzi ambapo jana bunge la taifa limeidhinisha majina ya wajumbe wa tume ya uchaguzi ikiwa ni mwezi mmoja kabla ya uchaguzi mkuu wa rais.

Jeremie Minani, msemaji wa vuguvugu la Arusha linalojumuisha vyama vya kisiasa na mashirika ya kiraia, amesema wanakemea kwa nguvu zote hatuwa ya serikali ya rais Nkurunziza na chama chake kuendelea kufanya mchezo wa kuigiza na kulazimisha mambo wakati tayari tume iliopo haikubaliki.

Wajumbe wawili kati ya watano wanaounda tume ya uchaguzi CENI ambao huteuliwa na rais na kuidhinioshw ana bunge, walijiuzulu na kuitoroka nchi, na kudhooofisha shughuli zote za tume ambapo uamuzi unatakiwa kuchukuliwa na wajumbe 4 kati ya 5.

Jumatatu juma hili ilitolewa sheria ya rais iliosainiwa Mei 30 iliobadilisha maamuzi kuchukuliw ana wajumbe 3 kati ya watano badala ya ilivyokuwa hapo awali wakati hapo jana jioni bunge la taifa liliidhinisha majinia ya wajumbe wawili kueneeza idadi ya wajumbe watano.

Msemaji huyo wa Vuguvugu la Arusha amesema uamuzi wa rais Nkurunziza ambae ni mgombea Urais kufanya mabadiliko ya mchezo wakati mechi ikiendelea, ni ishara dhihiri kwamba tume ya uchaguzi CENI ipo kwa ajili ya kumtengenezea Nkurunziza na chama chake kuendelea kufanya hujuma.

Mbali na kuidhinisha majina ya wajumbe hao wapya wa tume ya uchaguzi , mapema Ijumaa asubuhi wiki hii Tume huru ya Uchaguzi iliidhinisha majina ya wagombea wa nane wa uchaguzi mkuu wa rais, akiwemo rais wa sasa Pierre Nkurunziza , na kiongozi wa kihistoria wa chama cha FNL Agathon Rwasa pamoja na ma rais wawili wa zamani wa Burundi Sylvestre Ntibantunganya (1994-1996) na Domitien Ndayizeye (2003-2005).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.