Pata taarifa kuu
NIGERIA-CHAD-CAMEROON-BOKO HARAM-Usalama

Mapigano Diffa: hali ya hatari yaripotiwa

Serikali ya Niger imechukua uamzi, katika kikao cha baraza la mawaziri, Jumanne Februari 10, wa kutangaza hali ya hatari katika jimbo la Difaa.

Wanajeshi wa Chad katika mitaa ya Gambaru (Nigeria) Februari 4 mwaka 2015. Karibu wanajeshi 2,000 wa Chad huenda wakawasili Jumatano jioni wiki hii katika jimbo la Diffa (Niger) kwa kupambana dhidi ya Boko Haram.
Wanajeshi wa Chad katika mitaa ya Gambaru (Nigeria) Februari 4 mwaka 2015. Karibu wanajeshi 2,000 wa Chad huenda wakawasili Jumatano jioni wiki hii katika jimbo la Diffa (Niger) kwa kupambana dhidi ya Boko Haram. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Watu wengi walikamatwa Jumanne wiki hii. Wakati huohuo majeshi ya nchi zilizojikubalisha kuanzisha vita dhidi ya Boko Haram yamekua yakijiimarisha, huku Boko Haram ikiamua kutumia mikakati miwili muhimu: mashambulizi ya moja kwa moja na operesheni ya kutumia wanamgambo wake kwa kujilipua.

Serikali ya Niger imebaini kwamba hali ya hatari iliyotangaza itapelekea jeshi kutekeleza majukumu yake ya kutokomeza kundi la Boko Haram katika ukanda huo.

Hali hiyo ya hatari itatoa uwezo wa ziada kwa vikosi ambavyo vitakua kwenye uwanja wa mapambano. Hali hiyo itapelekea pia kwa vikosi hivyo kuendesha msako mchana kama usiku.

Mpaka sasa, kundi hilo la kigaidi limeendesha shambulio la moja kwa moja kwa kurusha mabomu, lakini pia kutumia wanamgambo wake kwa kujitoa mhanga, baada ya kupenya na kuingia katika mji, upande wa Niger.

Katika mkutano na vyombo vya habari Jumanne jioni wiki hii, Waziri mkuu Brigi Rafini, alitangaza kwamba vijana wa Niger, ambao walipewa mafunzo ya kijeshi katika kambi za Boko Haram, ndio wamekua wakiendesha mashambulizi nchini Niger.

Waziri mkuu wa Niger, amesema kwamba vijana wa jimbo la Difaa wameanza kujiandaa ili kuweka wazi harakati za kundi la Boko Haram. Katika maeneo mbalimbali ya jimbo hilo watu kadhaa walikamatwa Jumanne wiki hii.

Mbali na marufuku ya kutotoka nje, viongozi wa jimbo hilo wamepiga marufuku ya kuendesha pikipiki na baskeli katika jimbo hilo. Wanamgambo wa Boko Haram wamekua wakitumia pikipiki kwa kuendesha mashambulizi. Wawili miongoni mwa wanamgambo hao waliuawa Jumanne wiki hii na vikosi vya majeshi ya Nigeria katika mji wa Diffa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.