Pata taarifa kuu
NIGER-NIGERIA-CHAD-CAMEROON-BOKO HARAM-USALAMA

Niger: Boko Haram yashambulia Diffa

Wabunge wa Niger wametakiwa kupiga kura Jumatatu Februari 9 katika kukabiliana dhidi ya Boko Haram.  

Abubakar Shekau, kiongozi wa Boko Haram (kwenye mkanda wa video).
Abubakar Shekau, kiongozi wa Boko Haram (kwenye mkanda wa video). YouTube
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Niamey inataka kupeleka wanajeshi wake kujiunga na majeshi ya Chad, Cameroon na Nigeria ambazo ziko tayari kutokomeza kundi la Boko haram.

Hata hivyo Wabunge wa Niger wanapaswa kuidhinisha operesheni hiyo, wakati ambaponchi hiyo ililengwa na mashambulizi ya hivi karibuni ya Boko Haram.

Kundi hilo la Boko Haram liliendesha mashambulizi usiku wa Jumapili Februari 8 kuamkia Jumatatu Februari 9 dhidi ya jela la mji wa Diffa, karibu na mpaka wa Nigeria. Kkwa mujibu wa duru tuliyonazo, wapiganaji wa Boko Haram waliuawa, huku mwanajeshi wa Niger akijeruhiwa.

Mji wa Difaa ulishambuliwa mara mbili hivi karibuni. Mlipuko uliotokea katikati ya mji jana Jumapili uligharimu maisha ya mtu mmoja, na Jumatatu wiki hii, shambulio jipya lilishuhudiwa katika jengo la Idara ya forodha. Boko Haram ilijaribu kushambulia kuteka daraja muhimu la mji huo wa Diffa.

Kabla ya Bunge la taifa nchini Niger kuidhinisha kutumwa kwa wanajeshi wa Niger nchini Nigeria, Boko Haram imeendelea kurusha mabomu na maroketi katika mji wa Diffa. Lengo la mashambulizi hayo ni kuteka daraja hilo muhimu linalotumiwa kwa kuingia katika mji Diffa kwa kutoka Nigeria.

Wakati ambapo operseheni ya kikanda dhidi ya Boko Haram ikiandaliwa pamoja na kupitishwa kwa idhni ya Bunge la Niger, kiongozi wa Boko Haram, ameelezea msimamo wake katika mkanda wa video uliyorushwa Jumatatu wiki hii. Katika mkanda huo unaodumu dakika 28, Abubakar Shekau amekashifu zoezi hilo la kutumwa kwa wanajeshi kutoka mataifa hayo matatu.

“ Muungano wenu hautazaa matunda yoyote. Kwa hiyo mkusanye silaha zenu kwa kuweza kukabiliana na si: tunakutakieni mafanikio mema, karibuni”, amesema Shekau

Katika hotuba hii yenye uchokozi, kwa lugha ya Kiarabu na baadae kwa lugha ya Kihausa, kiongozi wa Boko Haram amesema kwa kauli ya dharau: " Mnatuma wanajeshi 7000? 7000 tu, kwa Mwenyezi Mungu ni idadi ndogo mno ! Tutawakama mmoja mmoja."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.