Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-AU-AFRIKA-BOKO HARAM-USALAMA

AU yazitaka chi za Afrika kukabiliana na Boko Haram

Wakati wa sherehe za ufunguzi wa Baraza la Mawaziri wa Umoja wa Afrika (AU) Jumatatu Januari 26, katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, mwenyekiti wa Tume ya shirikisho hilo, Nkosazana Dlamini-Zuma ametolea wito wito nchi za Afrika kujibu kwa pamoja dhidi ya tishio la Boko Haram.

Nkosazana Dlamini-Zuma, Oktoba 15 mwaka 2012, mjini Addis-Ababa
Nkosazana Dlamini-Zuma, Oktoba 15 mwaka 2012, mjini Addis-Ababa REUTERS/Tiksa Negeri
Matangazo ya kibiashara

Katika mkutano huo, kumezungumziwa hatua ya kiuchumi kwa kusaidia nchi zilioathirika na Ebola.

Kundi la Boko Haram limeendelea kuwa tishio, baada ya kuiteka miji kadhaa kaskazini magharibi mwa Nigeria, na sasa kundi hilo linatishia kuendelea na mapambano zaidi katika mji wa Maiduguri, mji mkuu wa Jimbo la Borno, mji wenye wakaazi zaidi ya milioni 2 ambako viongozi wamewatolea wito wananchi kuwa watulivu.

Kitisho hicho cha Boko Haram katika mji wa Maiduguri kimesababisha hofu kubwa miongoni mwa wananchi wakati huu wakijiandaa kuelekea kwenye uchaguzi wa urais mwezi ujao.

Kufuatia hali ilivyo kwa sasa kumekuwa na mitazamo tofauti kuhusu uchaguzi huo ambapo baadhi wameonya kuahirishwa kwa uchaguzi huo, huku upinzani ukiona kwamba hakuna sababu zozote za kuahirisha.

Marekani imeahidi kuisiadia Nigeria kupambana na kundi hilo wakati huu nchi hiyo ikijaindaa kwa uchaguzi wa urais mwezi ujao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.