Pata taarifa kuu
NIGERIA-CAMEROON-NIGER-BOKO HARAM-Usalama

Waathirika wa Boko Haram, watoa ushuhuda

Kundi la Boko Haram limeendelea na harakati zake za kutekeleza mashambulizi nchini Nigeria na nchi jirani, hususan Cameroon na Niger.

Rukaya alikamatwa na watoto wake wawili, ikiwa ni pamoja na mtoto mchanga wa miezi tisa.
Rukaya alikamatwa na watoto wake wawili, ikiwa ni pamoja na mtoto mchanga wa miezi tisa. RFI/ Nicolas Champeaux
Matangazo ya kibiashara

Wanafuzi zaidi ya 200 waliotekwa na kundi hilo mwezi Aprili katika shule ya Chibok, bado wanashikiliwa na kundi hilo. Baada ya tukio hilo, Boko Haram imeendelea na kitendo hicho cha utekaji nyara katika ukanda huo unaozijumuisha nchi kadhaa za Afrika Magharibi.

Mwezi Novemba kundi hilo liliwateka nyara zaidi ya wanawake na wasichana hamsini katika mji wa Damasak, kilomita kadhaa na mpaka wa Niger. Baadhi walifaulu kutoroka kundi hilo na kuvuka mpaka hadi katika kambi ya wakimbizi ya Chetimari, magharibi mwa mji wa Diffa, nchini Niger.

Waandishi wa habari wa RFI waliendesha uchunguzi na kufaulu kuongea na waathirika wa mashambulizi ya Boko Haram.

Adiza Abdou ana ishara laini na sahihi kuhusu vitendo alivyoshuhudia, ambavyo vilitekelezwa na Boko Haram, baada ya kuwateka watu katika mji wa Damasak.

Akivalia hijab yenye rangi ya zambarau akijifunika uso wake, huku macho yake akiyaacha nusu wazi bila kufunikwa, hali hiyo ikiwa inaeleza huzuni na utulivu.

Jumatatu Novemba 24 mwaka 2014, akiwa pamoja na mama yake na dada zake wakubwa Fatima, Bintou na Oumi, Adiza Abdou alikuwa akijiandaa kukimbia mashambulizi ya Boko Haram katika mji wa Damasak baada ya kutekwa nyara yeye na familia yake.

Wapiganaji wa Boko Haram, kwanza walimuua kijana mmoja mbele ya macho yao, kabla ya kuwachukua kwa nguvu na kuwaingiza katika gari lao na kuwapeleka wasikopajua. Adiza, mwenye umri wa miaka kumi na tatu, amesema alishuhudia ukatili wa wanamgambo wa Boko Haram, hususan kuua, kubaka na kutumia madawa ya kulevya. Adiza amebaini kwamba katika kundi la watu zaidi ya hamsini waliotekwa wakati huo, yeye ndiye alikuwa mwenye umri mdogo.

" Walituambia: kama mtathubutu kutusema, tutawakata vichwa. baadae walituambia: mwanamke anaweza kuolewa mara mbili, wala si haram. Tunafanya hivyo kwa sababu waume zenu si Waislamu wa kweli. Kisha walitueleza kwamba kuua watu wala si haram , kwa sababu hii ni sehemu ya majukumu aliyopewa Mtume", amethibitisha Adiza na familia yake.

Mateka walikua wakizuiliwa katika nyumba ya mkuu wa kijiji, aliye teuliwa na Boko Haram. Siku ya tatu, Adiza aliteuliwa na kuwekwa kando pamoja na wasichana wengine kumi na tano ambao walitakiwa kuolewa na wapiganaji wa kundi hilo la Boko Haram.

Adiza ameeleza kwamba, usiku huo, mama yake alifaulu kuwatorosha yeye na wasichana hao kumi na tano waliyokua wakitakiwa kuolewa na wapiganaji wa Boko Haram. Mama yake Adiza, Adiza mwenyewe na wasichana hao walivuka mto Yobe kwa kutumia mtumbwi na kukimbila katika nchijirani ya Niger. Adiza anakumbuka tukio hilo la kutoroka.

Wengi wa wanawake kwa wasichana waliokua wakishikiliwa mateka na Boko Haram wamethibitisha ukatili huo wa kundi Boko Haram, unaofayiwa wanawake na wasichana, huku wanaume na wavulana wakiuawa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.