Pata taarifa kuu
NIGERIA-MAREKANI-BOKO HARAM-Usalama

Boko Haram yauteka mji wa Monguno

Mji wa Monguno, kusini mashariki mwa Nigeria, umeshudiwa Jumapili Januari 25 asubuhi mapigano makali kati ya jeshi na wapiganaji wa kundi la Boko Haram.

Polisi wa Nigeria katika mji wa Maiduguri, katika jimbo la Borno, nchini Nigeria, wakati wa operesheni dhidi ya Boko Haram, mwezi Juni mwaka 2013.
Polisi wa Nigeria katika mji wa Maiduguri, katika jimbo la Borno, nchini Nigeria, wakati wa operesheni dhidi ya Boko Haram, mwezi Juni mwaka 2013. AFP PHOTO / Quentin Leboucher
Matangazo ya kibiashara

Jeshi liliingilia kati ili kukabiliana na kuzima mashambulizi ya Boko Haram katika mji wa Maiduguri, ambako kundi hilo lilikua likiendesha mashambulizi kwa lengo la kuyadhibiti maeneo yote ya mji huo

Hata hivyo wapiganaji wa Boko Haram waliuvamia na kuuteka mji mwengine wa Monguno katika jimbo la Borno.

Haya yanayotokea wakati huu, Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani John Kerrry akiwa ziarani nchini Nigeria.

Mwishoni mwa juma lililopita pia iliripotiwa kuwa, wapiganaji hao walijaribu kuiteka miji ya Maiduguri na Konduga kabla ya kushambuliwa na jeshi.

Kerry amekutana na rais Goodluck Jonathan na kiongozi wa upinzani Muhammadu Buhari mjini Lagos, na kuahidi kuwa nchi yake itaendelea kuisaidia Nigeria kupambana na Boko Haram.

Kuhusu Uchaguzi wa urais mwezi ujao, Kerry ameonya wale wanaopanga kufahdili na kuchochea machafuko baada ya Uchaguzi huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.