Pata taarifa kuu
CAMEROON-NIGERIA-Chad BOKO HARAM--Usalama

Mashambulizi ya Boko Haram: baadhi ya mateka waachiwa huru

Wapiganaji wa Boko Haram waliendesha mashamulizi Jumapili Januari 18 kaskazini mwa Cameroon. Zaidi ya wapiganaji mia moja walishambulia vijiji viwili viliyokaribu na mji wa Mokolo katika jimbo la kaskazini mwa Cameroon.

Wapiganaji wa Boko Haram katika mkanda wa Video, Aprili mwaka 2014.
Wapiganaji wa Boko Haram katika mkanda wa Video, Aprili mwaka 2014.
Matangazo ya kibiashara

Wapiganaji hao walifaulu kuwateka nyara zaidi ya watu themanini. Hata hivyo watu 24 miongoni mwa mateka hao waliachiliwa huru, baada ya majeshi ya Cameroon kujibu mashambulizi ya wapiganaji hao.

Mashambulizi hayo ya Boko Haram yaligharimu maisha ya watu watatu, huku uharibifu mkubwa ukishuhudiwa katika vijiji hivyo viwili. Zaidi ya nyumba 80 zilichomwa moto.

Baada ya kutimuliwa na jeshi la Cameroon, wapiganaji hao wa Boko Haram, walifaulu kupenya katika vijiji vya Mabassa na Maky, na kupora vitu na mali viliyokua ndani ya nyumba. Takriban watu 80 walitekwa nyara, lakini 24 miongoni mwao waliachiliwa huru.

Mashambulizi hayo yanatokea wakati ambapo Chad iliwatuma wanajeshi wake tangu Jumamosi Januari 17 mwaka 2015, ili kushiriki katika mpango wa kikanda wa kuendesha vita dhidi ya Boko Haram. Kwa mujibu wa msemaji wa serikali ya Cameroon, Issa Tchiroma Bakary, wapiganaji wa Boko garam wamekua wakivuka mpaka kwa minajili ya kutafuta chakula.

" Hali hiyo haitachukua muda mrefu, kwani nchi za ukanda huu zimeshikamana kwa kwa kulidhibiti kundi hilo”, amesema Issa Tchiroma Bakary.

Lengo la kutumwa kwa majeshi ya Chad ni kuurejesha mji wa Baga kwenye himaya ya serikali ya Cameroon. Mji wa Baga ni mji muhimu wa jimbo la kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.