Pata taarifa kuu
RWANDA-Sheria-Kanisa Katoliki

Rwanda: kifungo cha miaka 5 jela kwa kundi la waumini wa Kanisa katoliki

Watu wanane wa kundi la waumini wa Kanisa katoliki nchini Rwanda wamehukumiwa adhabu ya kifungo cha miaka mitano jela, wakituhumia kosa la kuhamasisha raia kwa lengo la kuanzisha vurugu.

Waumini wa Kanisa la katoliki wafungwa miaka mitano jela, baada kuonekana kuwa walitaka kumuigili rais Paul Kagame katika majukumu ya uongozi wake wa nchi.
Waumini wa Kanisa la katoliki wafungwa miaka mitano jela, baada kuonekana kuwa walitaka kumuigili rais Paul Kagame katika majukumu ya uongozi wake wa nchi. DR
Matangazo ya kibiashara

Baada ya Mahakama kuu mjini Kigali kutoa hukumu, Jaji wa Mahakama hiyo amebaini kwamba hukumu hiyo ni somo kwa wengine watakao kua na mwenendo kama huo.

“ Mtu yeyote ambayo atazagaza uvumi wenye lengo la kukuza vurugu, ajuwe kwamba ataadhibiwa kwa mujibu wa sheria.

Watu hao walikua wanakabiliwa na kifungo cha miaka 15 jela

Wakati kesi hiyo ikisikilizwa, watuhumiwa hao walibaini kwamba walishirikianana na Chantal Mutamba, baada ya kuwaambia kwamba alipata ufunuo wa Mungu unao watolea wito raia wa Rwanda kuacha "dhambi" au kujizuia kuporomosha mimba, la si hivo watakiona cha mtima kuni kuliko kile kilichotokea mwaka 1994 wakati wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda.

Kufuatia kesi hiyo, watuhumiwa wawili akiwemo Chantal Mutamba wameachiwa huru. Mahakam ilibani kwamba mtuhumiwa huyo alikua na tatizo la akili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.