Pata taarifa kuu
RWANDA-Sheria

Rwanda: Kizito Mihigo akabiliwa na kifungo cha maisha jela

Mwanamuziki maarufu nchini Rwanda, Kizito Mihigo kwa mara nyingine amekiri kuhusika na kupanga njama za kuwashambulia viongozi wa kitaifa kwenye serikali inayoongozwa na rais Paul Kagame.

Kizito Mihigo mbele ya vyombo vya habari, mjini Kgali Aprili 15 mwaka 2014, siku moja baada ya tangazo la kukamatwa kwake kutolewa.
Kizito Mihigo mbele ya vyombo vya habari, mjini Kgali Aprili 15 mwaka 2014, siku moja baada ya tangazo la kukamatwa kwake kutolewa. AFP PHOTO / STEPHANIE AGLIETTI
Matangazo ya kibiashara

Mihigo aliyasema haya wakati wa ufunguzi wa kesi yake alhamisi ya Juma hili ambapo aliwaambia majaji wanaosikiliza kesi yake kuwa kama alivyosema wakati akikamatwa na kuomba msamaha kuhusu tuhuma zinazomkabili, ndivyo anavyosisitiza tena wakati wa kesi yake.

Mwanamuziki huyo sambamba na wenzake wengine watatu wanashtakiwa na serikali ya Rwanda kwa tuhuma za kupanga njama za mauaji, ugaidi na uhaini dhidi ya Serikali ya rais Paul Kagame.

Kizito Mihigo na washukiwa wenzake wanakabiliwa na kifungo cha maisha jela.

Hata hivyo wakili wa Mihigo, John Bigaraba amesema kuwa serikali haina ushahidi wowote wa muhimu katika kesi inayomkabili Mihigo na wenzake Jean Paul Dukuzumuremyi ambaye ni mwanajeshi pamoja na waandishi wa habari, Cassien Ntamuhanga na Agnes Niyibizi ambao hawa wamekanusha mashtaka yao.

Kizito mihigo, ambaye alinusurika katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, alikamatwa Aprili 14 mwaka 2014, wiki moja baada ya familia yake kujua aliko.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.