Pata taarifa kuu
MALI

Waziri Mkuu mpya wa Mali aunda rasmi serikali ya nchi hiyo

Waziri mkuu mpya wa Mali Diango Cissoko ameunda rasmi serikali kamili ya nchi hiyo na kuteua mawaziri siku nne baada ya kumrithi waziri mkuu aliyejiuzulu kwa shinikizo Cheick Modido Diarra.

Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa viongozi walioteuliwa sasa ambao walikuwamo katika serikali ya Diarra ni pamoja na Waziri wa ulinzi Colonel Yamoussa Camara, Waziri wa mambo ya nje Tieman Coulibaly na waziri wa uchumi Tienan Coulibaly.

Serikali hiyo mpya inakabiliwa na changamoto ya kuhakikisha inaunganisha jeshi ambalo limekuwa likipata shinikizo kubwa toka kwa kiongozi aliyeongoza mapinduzi ya awali ya rais na waziri mkuu kapteni Amadou Sanogo.

Hivi karibuni jeshi hilo liliitoa kauli ya kutoridhia namna viongozi wa mataifa ya Afrika magharibi wanavyopanga kutuma majeshi ya ECOWAS kwa madai kuwa hata nao wana uwezo wa kupigana ikiwa watawezeshwa kwa fedha na silaha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.