Pata taarifa kuu
BAMAKO-MALI

Waasi wa Tuareg nchini Mali wasema mazungumzo ya awali na Serikali yameenda vizuri

Viongozi wa kundi la Tuareg lililojitangazia uhuru wake kaskazini mwa nchi ya Mali, wamesema kuwa mazungumzo yao na serikali mpya ya Mali yameenda vizuri. 

Rais wa Mpito wa Mali, Diouncounda Traore (katikati) akizungumza na Captain Amadou Haya Sanogo (kushoto) aliyeoongoza mapinduzi nchini humo
Rais wa Mpito wa Mali, Diouncounda Traore (katikati) akizungumza na Captain Amadou Haya Sanogo (kushoto) aliyeoongoza mapinduzi nchini humo Reuters/Joe Penney
Matangazo ya kibiashara

Hamma Ag Mahmoud mjumbe wa tawi la chama cha Azawad National Liberation Movement MNLA, amesema kuwa mara baada ya mazungumzo yao ya awali na serikali yameonesha kuzaa matunda ambayo yatapelekea kuoatikana kwa suluhu.

Juma moja lililopita waasi hao wa Tuareg alijitangazia uhuru wa taifa lao jipya waliloliita Azawad wakati kukiwa na mgogoro wa kimadaraka nchini humo kufuatia mapinduzi ya kijeshi.

Rais wa mpito wa Mali, Diancounda Traore mara baada ya kuapishwa aliwataka waasi hao kuja kwenye meza ya mazungumzo na serikali huku akitishia kutumia nguvu za kijeshi kuwasambaratisha iwapo wangekataa kutekeleza amri yake.

Serikali mpya ya Mali imeomba msaada toka serikali ya Mauritania kwaajili ya kusimamia mazungumzo hayo na kundi hilo.

Nchi ya Mali ilikumbwa na mapinduzi ya kijeshi mwishoni mwa mwezi uliopita na wanajeshi waliodai serikali ya rais Toure ilishindwa kushughulikia vema mgogoro uliokuwa ukiendelea kaskazini mwa nchi ya Mali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.