Pata taarifa kuu
MALI

Rais wa Mali Toure amejiuzulu kupisha mpango wa kurejesha amani nchini mwake

Rais aliyeondolewa madarakani nchini Mali kwa mapinduzi yasiyomwaga damu ya Kijeshi Amadou Toumani Toure amejiuzulu wadhifa wake ikiwa ni sehemu ya mapendekezo ya utekelezaji wa mpango wa amani katika nchi hiyo uliopendekezwa na Viongozi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Magharibi ECOWAS.

Rais aliyeondolewa madarakani nchini Mali Amadou Toumani Touré ambaye ametangaza kujiuzulu
Rais aliyeondolewa madarakani nchini Mali Amadou Toumani Touré ambaye ametangaza kujiuzulu Guillaume Thibault/RFI
Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa Nchi wanachama wa ECOWAS walifikia hatua ya kumtaka Rais Toure kukaa kando ili kuruhusu mpango wa kurejesha amani katika nchi hiyo ambayo imejikuta kwenye matatizo baada ya Wanajeshi wakiongozwa na Kapteni Amadou Haya Sanogo kutekeleza mapinduzi.

Rais Toure amesema hiyo ni hatua nzuri sana iliyofikiwa na ECOWAS katika kurejesha hali ya utulivu nchini Mali baada ya kushuhudia majuma zaidi ya matatu ya hali tete ndani ya nchi hiyo iliyo na histori ya kushuhudia mapinduzi ya kijeshi.

Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi ECOWAS ililazimika kufanya mkutano wa pande zinazosigana nchini mali ambapo mwisho wakakubaliana ni lazima Rais Toure akae kando ili kuweza kufanikisha mpango wa kurejesha amani kwenye nchi hiyo inayozidi kugawanyika.

Rais Toure amesema kuwa huu unaweza ukawa mwanzo wa kuimarisa demokrasia katika nchi hiyo ambayo imekuwa ikipambana katika kuhakikisha wananchi wa Taifa hilo wanashikamana katika kipindi hiki cha mpito.

Kujiuzulu kwa Rais Toure kunatoa nafasi kwa Spika wa Bunge Dioncounda Toure kuongoza nchi hiyo kwa kipindi hiki cha mpito kabla ya kuitisha uchaguzi ambao unatarajiwa kufanyika katika kipindi cha siku arobaini zijazo.

Mazungumzo hayo hayakuweka bayana kama juhudi hizo zitagusa eneo la Kaskazini hasa Mji wa Azawad ambao upo chini ya Waasi wa Tuareg wanaomiliki Kundi la MNLA ambao wametangaza rasmi uhuru wa sehemu hiyo.

Rais wa Burkina Faso Blaise Compaore ni miongoni mwa waliofanyakazi kubwa katika kuhakikisha suala hili linafanikiwa na akatoa wito wa kuheshimiwa kwa katiba ya nchi hiyo ili kuepukana na mapinduzi ya kijeshi.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki Moon na Kiongozi wa kanisa Katoliki Duniani Papa Benedict XVI wametaka utulivu urejeshwe nchini Mali pamoja na kutekelezwa kwa mapendekezo ya amani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.