Pata taarifa kuu
ARMENIA-SIASA

Wabunge washindwa kumchagua waziri mkuu mpya Armenia

Bunge la Armenia limeshindwa kumchagua Waziri Mkuu mpya,baada ya kuwa na kikao cha dharura kujadili hali ya kisiasa nchini humo.

Wafuasi wa Nikol Pachini walikusanyika kwenye eneo la Jamhuri mjini Erevan baada ya kushindwa kuchaguliwa kama waziri mkuu, Mei 1.
Wafuasi wa Nikol Pachini walikusanyika kwenye eneo la Jamhuri mjini Erevan baada ya kushindwa kuchaguliwa kama waziri mkuu, Mei 1. REUTERS/Gleb Garanich
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii ilikuja baada ya kujiuzulu kwa Waziri Mkuu wa zamani Serzh Sargsyan wiki iliyopita, baada ya wiki mbili za maandamano kumtaka kujiuzulu.

Kuelekea kikao hicho, ilikuwa wazi kuwa wabunge wangemchagua kiongozi wa upinzani Nikol Pashinyan,kushikilia nafasi hiyo.

Baada ya kutofanikiwa, kwa zoezi hilo kiongozi huyo wa upinzani amewashtumu wabunge wa Republican kwa kukataa kumuunga mkono bungeni.

Kutokana na hali hii, kiongozi huyo wa upinzani ameitisha mgomo na maandamano ya kitaifa hivi leo kulaani hatua hiyo ya baadhi ya wabunge ambayo ameilezea kama matusi kwa watu wa Armenia.

Kiongozi wa upinzani Nikol Pachini akiwapa kofia wafuasi wake kwenye eneo la Jamhuri huko Erevan mnamo Aprili 30, 2018.
Kiongozi wa upinzani Nikol Pachini akiwapa kofia wafuasi wake kwenye eneo la Jamhuri huko Erevan mnamo Aprili 30, 2018. REUTERS/Gleb Garanich

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.