Pata taarifa kuu
MAREKANI-SIASA

Obama na Bush walaani siasa za mgawanyiko nchini Marekani

Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama ameonekana kurejea kwenye ulingo wa kisiasa baada ya kushtumu siasa za mgawanyiko ambazo amesema zinaendelea nchini humo.

Marais wa zamani wa Marekani (George W. Bush na Barack Obama) wanamshutumu rais wa sasa Donald Trump kuweka mbele siasa za mgawanyiko.
Marais wa zamani wa Marekani (George W. Bush na Barack Obama) wanamshutumu rais wa sasa Donald Trump kuweka mbele siasa za mgawanyiko. SAUL LOEB / AFP
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza katika jimbo la New Jersey alipokwenda kumuunga mkono mgombea wa Ugavana kupitia chama cha Democratic, Obama amesema uongozi wa rais wa sasa Donald Trump, unaeneza siasa za uoga ambazo amesema zimepitwa na wakati.

Barack Obama amewataka wapiga kura kukataa kile alichokitaja kuwa siasa za kuwagawanya watu mbali na siasa za hofu.

Obama amesema haya siku chache baada ya rais Trump kumtuhumu kuwa alikuwa hawapigii simu wanajeshi walio nje ya nchi hiyo.

Matamshi yake yanajiri saa chache baada ya mtangulizi wake George W. Bush kukosoa unyanyasaji na chuki katika maisha ya kawaida ya raia wa Marekani.

“Chuki dhidi ya wale wanaokupinga zimeongezwa nguvu huku maadili ya kiraia yakisahaulika” alisema George W. Bush katika hotuba yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.