Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI SIASA

Askofu Mkuu wa Cape amkosoa Jacob Zuma katika hotuba yake

Nchini Afrika Kusini, kama kawaida kila mwaka, Askofu Mkuu wa Cape Town ametoa mahubiri ya kisiasa kwa siku ya Krismasi Jumapili hii Desemba 25. Askofu Mkuu Thabo Makgoba kutoka kanisa la Anglikani, ni mmoja wa warithi wa Desmond Tutu.

Thabo Magkoba hapa katika Jukwaa la Uchumi Duniani lililofanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia, mwezi Mei 2012.
Thabo Magkoba hapa katika Jukwaa la Uchumi Duniani lililofanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia, mwezi Mei 2012. World Economic Forum [CC BY-SA 2.0]/Wikimedia Commons
Matangazo ya kibiashara

Askofu Magkoba ni kiongozi wa kidini ambaye amejikita sana katika siasa za Afrika Kusini. Wakati wa hotuba yake, Thabo Makgoba alimjibu Rais Jacob Zuma, ambaye anataka viongozi wa kidini kutojihusisha na siasa.

Nci ya Afrika Kusini inakabiliwa na "mtafaruku wa kisiasa", kwa mujibu wa Askofu Mkuu wa Cape Town. "Inaonekana kwamba tuko katika miaka ya 1963, stukiishi katika hali ya hatari iliyowekwa na viongozi wanaojihusisha rushwa ambao wametusahau," alisisitiza Thabo Magkoba.

Askofu Mkuu wa Cape Town hajasita kumkosoa Jacob Zuma na viongozi wa chama tawala cha ANC (African National Congress). Kwa mujibu wa Thabo Magkoba, viongozi wa kidini wana nafasi ya kubwa katika siasa ya nchi, Askofu Thabo magkoba amemuonya Jacob Zuma: "Mheshimiwa rais, Tutapuuzia wito wako, unaoutoa ukiwa madarakani, ambapo wewe na marafiki zako mnaishi kwa furaha na faraja. Tutaendelea mapambano haya kwa kutetea uhuru na kwa upatikanaji wa fursa, na usawa wa kiuchumi uimarike. "

Kwa mujibu wa Askofu Magkoba, demokrasia iko imara, lakini "Serikali imedhoofika"

ANC "inakabiliwa na mgawanyiko wa ndani", na" Serikali imedhoofika, " askofu mkuu wa cape Town amesema. "Katika hatua gani, makanisa, misikiti na masinagogi, tunapaswa kujiondoa kutoa mchango wetu kwa serikali iliyochaguliwa? "askofu Magkoba ameuliza.

Licha ya mahubiri haya, Askofu Mkuu wa Cape Town alikaribisha demokrasia ya Afrika Kusini akisema bado ina nguvu na iko imara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.