Pata taarifa kuu
RAGA

Kenya yataja kikosi cha kushiriki michuano ya irb nchini Marekani na Canada

Kocha wa timu ya taifa ya mchezo wa raga ya Kenya yenye wachezaji 7 kila upande Innocent Simiyu , amewaacha wachezaji Oscar Ouma na Brian Tanga katika kikosi chake cha mwisho kuelekea katika makala ya sita na tano kuwania ubingwa wa michuano ya dunia ya HSBC .

Kikosi cha Kenya katika michuano iliyopita ya irb sevens
Kikosi cha Kenya katika michuano iliyopita ya irb sevens www.worldrugby.org
Matangazo ya kibiashara

Mzunguko wa kwanza wa michuano hiyo itafanyika jijini Las Vegas nchini Marekani kati ya tarehe 3 hadi 5 mwezi Machi huku mchuano mwingine ukifanyika jijini Vancouver nchini Canada kati ya tarehe 11 na 12 mwezi Machi.

Frank Wanyama na Oscar Ayodi ni wachezaji wengine waliorejea katika kikosi cha taifa.

Kikosi kamili ni: William Ambaka, Dan Sikuta,Frank Wanyama, Eden Agero, Augustine Lugonzo, Billy Odhiambo, Collins Injera, Nelson Oyoo, Leonard Mugaisi, Oscar Ayodi, Bush Mwale na Samuel Oliech.

Jijini Las Vegas nchini Marekani, Kenya imejumuisha katika kundi la C pamoja na New Zealand, Argentina na Urusi.

Makundi mengine, kundi la A:- Afrika Kusini, Wales, Ufaransa na Canada .

Kundi B: Uingereza, Marekani, Samoa na Chile.
Kundi D: Australia, Fiji, Japan na Scotland.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.