rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Kenya

Imechapishwa • Imehaririwa

Kenya: Moto wateteketeza soko kuu Mjini Nairobi

media
Wafanyabiashara katika soko la Toi wameelezea masikitiko yao, huku wakibaini kwamba wamepoteza mamilioni ya fedha. http://www.muungwana.co.tz

Soko la Toi mjini Nairobi, chini Kenya, limeteketea kwa moto alfajiri ya Jumanne hii Machi 12 na kuteketeza mali ya thamani isiyojulikana. Moto huo umezuka kwenye majira ya saa tisa alfajiri katika soko hilo.


Soko la Toi ni soko maarufu linalofahamika kwa uuzaji wa bidhaa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukuu, nguo za mtumba, lakini pia bidhaa nyingine kama mbao na vifaa vya elektroniki.

Baadhi ya wafanyabiashara wamelaumu idara za zima zoto kuchelewa kukabiliana na moto huo kwa wakati mzuri na kuudhibiti kabla ya kusambaa katika sehemu nyingine. Idara ya zima Moto nchini Kenya imekuwa ikishtumiwa kwa kushindwa kudhibiti mikasa ya moto kwa muda muafaka na licha ya kuwa na vifaa vipya.

Hata hivyo chanzo kutoka idara ya zima moto kikiniukuliwa na BBC kimesema kuwa magari ya zima moto yameshindwa kuingia ndani zaidi katika soko hilo kutokana na makazi yasiyo rasmi kama vijiji yanakuwa hayana mpangilio mzuri, nyumba husongamana sana na hakuna njia za katikati.

Wafanyabiashara katika soko hilo wameelezea masikitiko yao, huku wakibaini kwamba wamepoteza mamilioni ya fedha, na kusema walitegemea biashara katika soko hilo kujikwamua kimaisha.