Pata taarifa kuu
KENYA

Mashaka yatanda uchaguzi mpya Kenya

Hali ya mashaka inaongezeka kuhusu uwezo wa Kenya kufanya uchaguzi mpya wa rais ndani ya mwezi mmoja wakati huu wahusika muhimu wakishindwa kukubaliana kuhusu namna ya kufanya uchaguzi wa kuaminika, wachambuzi wanasema.

David Maraga jaji wa mahakama ya juu nchini Kenya
David Maraga jaji wa mahakama ya juu nchini Kenya REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Kutokukubaliana kwa pande zote na sintofahamu iliyopo kuhusu mchakato huo wa uchaguzi mpya kumeongezeka tu mara baada ya tume ya uchaguzi kutangaza tarehe 17 Oktoba kuwa tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi huo baada ya ule wa awali kufutwa.

 

Upinzani nchini Kenya umeapa kusuia uchaguzihuo ikiwa orodha yake ya madai haitashughulikiwa, ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya wafanyakazi katika tume ya uchaguzi (IEBC), ambao upinzani unawashutumu kuvuruga uchaguzi.

Mwanaharakati maarufu wa kupambana na rushwa nchini Kenya, John Githongo amesema kuwa changamoto zilizopo si za kawaida kabisa akisema kuwa tarehe ya uchaguzi "haionekani kuwa inawezekana kwa sababu tunawataka watu ambao wameshindwa kabisa, kuandaa uchaguzi baada ya muda mfupi kiasi hicho.

Kikwazo muhimu ni kwamba Mahakama Kuu bado haijatoa hukumu yake kamili kueleza kwa nini hasa iliamua kufuta ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta.

Jaji Mkuu David Maraga alitaja tu dosari na makosa ya kinyume na sheria, hasa katika kuhamisha matokeo ya uchaguzi.

Mahakama ina hadi Septemba 22 kutoa hukumu kamili, ambayo inaweza kuipa IEBC muda kidogo wa kufanya mabadiliko yoyote muhimu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.