Pata taarifa kuu
LIBYA-MAPIGANO-USALAMA

Libya: Thelathini na mbili waangamia katika mapigano Libya

Mapigano yanaendelea karibu na mji mkuu wa Libya, Tripoli, kati ya majeshi ya Marshal Khalifa Haftar na vikosi vya serikali ya umoja wa kitaifa inayoungwa mkono na jumuiya ya kimataifa.

Wapiganaji wa kundi la ANL yanayoongozwa na Marshal Khalifa Hafta, yakiondoka Benghazi na kuam kuwasadia wenzao wanaoelekea Tripoli, Benghazi, Libya, Aprili 7, 2019.
Wapiganaji wa kundi la ANL yanayoongozwa na Marshal Khalifa Hafta, yakiondoka Benghazi na kuam kuwasadia wenzao wanaoelekea Tripoli, Benghazi, Libya, Aprili 7, 2019. REUTERS/Esam Omran Al-Fetori
Matangazo ya kibiashara

Mapigano hayo yaliyozuka tangu Jumamosi yameua watu zaidi ya arobaini kwa mujibu wa mashahidi.

Kwa siku tu ya Jumapili Aprili 7, watu 21 wameuawa katika mapigano hayo ambapo ndege za kivita zilitumiwa kwa pande zote.

Kiongozi wa majeshi hayo yanayodhibiti eneo la mashariki mwa Libya Marshal Khalifa Haftar ameapa kuingia Tripoli, mji unaodhibitiwa na majeshi ya serikali ya umoja wa kitaifa inayoungwa mkono na jumuiya ya kimataifa.

Uongozi wa majeshi ya Khalifa Haftari umethibitisha kwamba magari kadhaa ya maadui yameharibiwa vibaya na mashambulizi ya angani yaliyoendeshwa na vikosi vya kiongozi huyo karibu na mji wa Tripoli.

Hata hivyo vyombo vya habari vya Libya vimehakikisha kwamba uharibifu au hasara ilikuwa ndogo ikilinganishwa na ukubwa wa mapigano hayo ambako ndege za kivita zilitumiwa kwa pande zote.

Umoja wa Mataifa umejaribu kushinikiza pande husika katika mapigano hayo kusitisha mapigano kati ya saa kumi hadi saa kumi na mbili jioni jana Jumapili ili kuweza kuondoa raia wa kawaida, bila mafanikio.

Makundi ya wanamgambo kutoka Zahouia, Misrata na Zliten wanaounga mkono serikali ya Tripoli yamewasili katika mji huo. Wamekuja kukabiliana na majeshi ya Marshal Khalifa Haftar.

Marekani imezitaka pande zinazokinzana kusitisha mapigano hayo haraka iwezekanavyo.

Awali Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo, alisema kuwa Marekani ina wasiwasi na mapigano hayo karibu na mji wa Tripoli.

Wakazi wa mji wa Tripoli wameingiliwa na uoga na wasiwasi, wakiomba Umoja wa Mataifa kuingilia kati ili kukomesha mapigano hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.