Pata taarifa kuu
LIBYA-MAZUNGUMZO-SIASA-USALAMA

Mkutano wa kutafutia suluhu mgogoro wa Libya kufanyika Palermo

Italia, iliyoitawala Libya wakati wa enzi za ukoloni, inatarajia Jumatatu wiki hii kuanzisha mkutano wa kimataifa huko Palermo ili kujaribu kutafuta suluhu mgogoro wa kisiasa unaoikabili Libya na kuanzisha mchakato wa uchaguzi mwaka ujao. Mkutano huu unafanyika baada ya ule wa Paris mwezi Mei mwaka huu.

Vikosi vya ulinzi tiifu kwa serikali inayotambuliwa kimataifa vikipambana dhidi ya kundi la watu wenye silaha Tripoli, Septemba 22, 2018.
Vikosi vya ulinzi tiifu kwa serikali inayotambuliwa kimataifa vikipambana dhidi ya kundi la watu wenye silaha Tripoli, Septemba 22, 2018. © REUTERS/Hani Amara
Matangazo ya kibiashara

Lengo la serikali ya Italia katika mkutano huu wa Palermoni kujaribu kukutanisha pande husika katika mgogoro huo na kuendelea kufuatialia hatua kwa hatua jinsi hali inavyoendelea nchini humo. Suala hili limechukuliwa moja kwa moja na serikali na sio Wizara ya Mambo ya Nje.

Mkutano huo ni muhimu kwa Italia. Kando na jitihada hizi za kuunga mkono mchakato wa amani nchini Libya, kuna suala la kimkakati kuhusu wahamiaji wanaoingia nchini Italia wakitokea katika Pwani ya Libya. Hata hivyo haijajulikana iwapo Jenerali Khalifa Haftar atashiriki kwenye mazungumzo hayo.

Kiongozi wa serikali ya umoja nchini Libya. Fayez al-Sarraj, Aguila Saleh, Spika wa Bunge na Khaled al-Mishri, mkuu wa baraza la usalama la Tripoli watashiriki kwenye mazungumzo hayo. Marais wa Ufaransa, Urusi na Marekani pamoja na Kansela wa Ujerumani wamekataa kushiriki mazungumzo hayo, lakini watawakilishwa maafisa wa sera za kigeni.

Rais wa Tunisia, wajumbe kadhaa kutoka Uturuki, Algeria, Morocco au Qatar na Federica Mogherini kwa niaba ya Umoja wa Ulaya na Ghassan Salameh kwa niaba ya Umoja wa Mataifa pia watahudhuria mkutano huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.