Pata taarifa kuu

Rais: Putin atoa wito kwa Warusi kuonyesha 'uzalendo' na kuja kupiga kura

Rais wa Urusi Vladimir Putin siku ya Alhamisi ametoa wito kwa watu wake kuonyesha "uzalendo" kwa kupiga kura katika uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika Machi 15 hadi 17 nchini Urusi.

Le président russe Vladimir Poutine, lors d'un discours à Chelyabinsk, en Russie, le 16 février 2024.
Rais wa Urusi Vladimir Putin wakati wa hotuba yake huko Chelyabinsk, Urusi, Februari 16, 2024. AP - Ramil Sitdikov
Matangazo ya kibiashara

"Ninawaomba mwende kupiga kura na kueleza msimamo wenu wa kiraia na uzalendo, kumpigia kura mgombea uliyemchagua, kwa mustakabali mzuri wa Urusi yetu tunayoipenda," Bw. Putin amesema katika hotuba ya video, iliyorushwa kwa televisheni ya umma.

"Kushiriki katika uchaguzi leo ni kuonyesha hisia zenu za kizalendo," amesisitiza.

Hayo yanajiri wakati mataifa wanachama wa Umoja wa Ulaya yamekubaliana kuipatia Ukraine msaada zaidi wa kijeshi wa dola bilioni 5.5.

Ubelgiji ambayo sasa ni mwenyekiti wa umoja huo imesema mabalozi kutoka mataifa hayo 27 wamekubaliana kimsingi juu ya mpango wa kusaidia upelekaji wa silaha nchini Ukraine.

Mchango huo utaingizwa kwenye mfuko unaoratibiwa na Umoja wa Ulaya wa European Peace Facility.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dymitro Kuleba ameyaita makubaliano hayo kuwa ya muhimu ya yaliyofikiwa kwa wakati muafaka.

Uamuzi wa kuongeza ufadhili ulicheleweshwa kwa miezi kadhaa kutokana na mvutano miongoni mwa wanachama juu ya namna utakavyotumika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.