Pata taarifa kuu

Ukraine: Ndege zisizo na rubani zatekeleza mashambulizi Kyiv na jimbo lake

Nchini Ukraine, Kyiv na jimbo lake vimekumbwa na mashambulizi makubwa ya ndege zisizo na rubani za Urusi usiku kucha na Jumamosi hii asubuhi. Hili ni shambulio kubwa zaidi tangu uvamizi wa mwezi wa Februari 2022 kulingana na mamlaka ya Ukraine. 

Ukraine: Wazima moto wakiwa kazini kuzima moto uliosababishwa na ndege zisizo na rubani za Shahed zilizoanguka usiku wa Novemba 24 kuamkia 25 huko Kyiv na jimbo lake.
Ukraine: Wazima moto wakiwa kazini kuzima moto uliosababishwa na ndege zisizo na rubani za Shahed zilizoanguka usiku wa Novemba 24 kuamkia 25 huko Kyiv na jimbo lake. AFP - HANDOUT
Matangazo ya kibiashara

 

Ukraine inaishutumu Moscow kwa kufanya shambulio lake kubwa zaidi la ndege zisizo na rubani dhidi ya Kiev usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi dhidi ya nchi hiyo mnamo mwezi wa Februari 2022. Jeshi la wanahewa la Ukraine limehakikisha Jumamosi hii asubuhi kwamba limeangusha ndege 71 zisizo na rubani za Shahed, zilizorushwa na Urusi. "Ndege nyingi zimeharibiwa katika jimbo la Kyiv," jeshi la Ukraine limesema kwenye mitandao ya kijamii.

Usiku ulikuwa mrefu, anaripoti mwandishi wetu huko Kyiv, Emmanuelle Chaze. Tuliamshwa katika mji wa Kyiv saa za mapema na milipuko ya mfululizo kwa saa moja. Tulisikia kazi ya mfumo wa ulinzi wa anga wa Ukraine ukipambana dhidi ya ndege zisizo na rubani zilizoingia kwenye mji mkuu kwa mawimbi kadhaa. Kwa nini mawimbi kadhaa? Kwa sababu ndege ya kwanza ilitumwa kwa mara ya kwanza kuwezesha askari wa Urusi kupata maeneo yaliyoko mfumo wa ulinzi wa anga wa Ukraine pia wakijaribu kuulenga na kuuharibu. Lengo lingine la shambulio la Urusi ni miundombinu muhimu ya Ukraine, miundombinu ya nishati hasa, na maeneo ya kijeshi pia. Isipokuwa kwamba, wakati ndege hizi zisizo na rubani zikinaswa juu ya anga ya mji mkuu, huanguka kwenye maeneo ya makazi.

"Kwa sababu hiyo, majengo 77 ya makazi na majengo 120 katikati mwa jiji hayana umeme," ilisema Wizara ya Nishati asubuhi, ili kuhakikisha kuwa kazi ya ukarabati inaendelea. 

Kulingana na mamlakahuko Kyiv, watu watano akiwemo mtoto wa miaka 11 wamejeruhiwa wakati wa mashambulizi ya Urusi. Tahadhari ya anga katika mji mkuu ilidumu kwa saa sita na mabaki ya ndege yanayoanguka kutoka kwa ndege zisizo na rubani yalisababisha moto na majengo yaliyoharibiwa katika mji mkuu, Meya wa Kiev Vitali Klitschko amesema. "Adui anaendelea kuwa na hofu," ameongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.