Pata taarifa kuu

Kremlin yakiri uwepo wa vikosi vya Ukraine kwenye ukingo unaodhibitiwa na Urusi wa Dnieper

Kwa mara ya kwanza, Urusi inatambua uvamizi wa Ukraine kwenye ukingo unaokaliwa wa Dnieper, katika mkoa wa Kherson. Habari hiyo imethibitishwa na jeshi la Ukraine. Mnamo Novemba 16, shambulio jipya la anga katika mkoa wa Kherson lilisababisha kifo cha mtu mmoja.

Urusi ilitambua mnamo Novemba 15 uvamizi wa Ukraine kwenye ukingo unaokaliwa wa Dnieper, mto ulio karibu na Kherson, moja ya vizuizi vyake muhimu vya kimkakati.
Urusi ilitambua mnamo Novemba 15 uvamizi wa Ukraine kwenye ukingo unaokaliwa wa Dnieper, mto ulio karibu na Kherson, moja ya vizuizi vyake muhimu vya kimkakati. AP - Alex Babenko
Matangazo ya kibiashara

Kutoka kwa mwandishi wetu maalum huko Mykolayev,

Warusi wenyewe wanakiri: Wanajeshi wa Ukraine wako kwenye ukingo huu unaokaliwa wa Dnieper, kama kilomita 35 kutoka mji wa Kherson, katika eneo la Khrynky. Hii imethibitishwa kwa upande wa Ukraine na Natalia Houmeniouk, msemaji wa Kamandi ya Kusini ya jeshi la Ukraine, ambaye ametangaza kwamba ni eneo la mapigano linalotumika kwa kilomita kadhaa.

Huu sio uvamizi wa kwanza wa Ukraine upande huu. Tangu mwezi wa Februari, kumekuwa na ongezeko la wanajeshi wa Ukraine kuingia katika eneo hili, hali iliyozidi kuimarika hata tangu majira ya joto, tangu mwezi Agosti 2023. Lakini haijawahi kuwa na uthibitisho kutoka upande wa Urusi. Ugumu kwa Waukraine itakuwa kusimamia kupata wanajeshi na vifaa vya kutosha katika ukingo hu unaomilikiwa na Urusi hatimaye kuvunja safu hii ya ulinzi. Na kama hii itatokea, kuwa na uwezo wa kuzima mashambulizi ya Urusi ambayo ilizindua kutoka ukingo wa upande wa pili, hasa, mji uliokombolewa wa Kherson. Kwa kweli ni ngumu sana kwa jeshi la Ukraine kusonga mbele chini ya mizinga ya Urusi na bila kuwa na silaha za kudungua ndege za kivita au kuwa ndege za kivita ambavyo Warusi wanavyo. Kwa hiyo hii ni habari ya kuchukuliwa kwa tahadhari.

Kituo cha jiji kililengwa mnamo Jumatano Novemba 15. Miundombinu ya raia imeathirika na kuharibiwa. Maktaba ziliharibiwa mapea wiki hii. Kuna vifo karibu kila siku, katika jiji la Kherson na pia katika eneo hilo. Kila siku, raia wanajeruhiwa. Siku ya Jumanne, mtoto wa miezi miwili na mama yake waliangamia wakiwa katika gari lao katika shambulio la anga la Urusi.

Ukraine, le 15 novembre 2023: troupes ukrainiennes camouflΓ©es dans la rΓ©gion de
Ukraine, Novemba 15, 2023: Wanajeshi wa Ukraine wakijificha katika eneo la Zaporizhia, kwenye uwanja wa vita. REUTERS - STRINGER
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.