Pata taarifa kuu

Volodymyr Zelensky aishutumu Moscow kwa kuunga mkono Hamas

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amezungumza katika mahojiano kwenye teevisheni ya France 2 kuhusu hali ya sasa ya Ukraine, lakini pia Israel na Palestina. Alipoulizwa kuhusu kutokuwa na uhakika kuhusu kuendelea kwa misaada ya Marekani kwa nchi yake dhidi ya hali ya mzozo wa kisiasa nchini Marekani, Volodymyr Zelensky amesema anatumai kwamba msaada huu "utaendelea" kutolewa.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky katika makao makuu ya NATO, Oktoba 11, 2023.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky katika makao makuu ya NATO, Oktoba 11, 2023. AP - Olivier Matthys
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameishutumu Urusi kwa "kuunga mkono" mashambulizi yanayofanywa na Hamas nchini Israel, akihofia kwamba vita hivi vipya vitavuruga tahadhari ya kimataifa kutokana na kile kinachotokea Ukraine, wakati wa mahojiano kwenye televisheni ya France 2 yaliyorushwa hewani siku ya Jumanne jioni. "Tuna hakika kwamba Urusi inaunga mkono, kwa njia moja au nyingine, shughuli zinazofanywa na Hamas," alisema Volodymyr Zelensky, akiongeza kwamba idara zake za kijasusi zilikuwa na "taarifa" kwa shambulio hilo.

Urusi inatafuta sana kuzorotesha usalama duniani

"Mgogoro wa sasa (...) unashuhudia ukweli kwamba Urusi inatafuta kweli kutekeleza vitendo vya kuzorotesh usalama wa dunia," amesema. Kiongozi huyo wa Ukraine pia ameelezea wasiwasi wake kuona jumuiya ya kimataifa ikiiacha Ukraine kutokana na "janga" ambalo linaikumba Israel kufuatia mashambulizi ya Hamas. Kwa jumla, vita hivyo tayari vimesababisha vifo vya zaidi ya watu 3,000 kwa pande zote mbili, raia, wanajeshi wa Israel na wapiganaji wa Hamas.

"Nisingependa kulinganisha hali hii. Vita vya kutisha vinaendelea katika nchi yetu. Katika Israeli, watu wengi wamepoteza wapendwa wao. Hali ni tofauti kabisa, lakini yote ni misiba mikubwa," amesema. Hata hivyo, ameonya kwamba "nia ya kimataifa inahatarisha kujisahauisha na Ukraine, na hii itakuwa atahri mbaya."

Mpango huo uko upande wetu hivi sasa

Kuhusu kuendelea kwa vita nchini Ukrainia, Volodymyr Zelensky alithibitisha kwamba mashambulizi yaliyoanzishwa na jeshi lake mwezi Juni kujaribu kuyakomboa maeneo yaliyokaliwa "yanaendelea, na kwa hali zote, tunasonga mbele".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.