Pata taarifa kuu

Moscow (diplomasia): Ukraine ilisaidiwa na London na Washington kushambulia Crimea

Mashambulizi ya anga ya Ukraine ya Septemba 22 kwenye makao makuu ya kikosi cha wanamaji cha Urusi kwenye Bahari Nyeusi huko Crimea "yalitekelezwa kwa ombi la idara za kijasusi za Marekani na Uingereza" na kuratibiwa nchi hizo, diplomasia ya Urusi imeshtumu Jumatano Septemba 27.

Meli ya Urusi iliyoharibiwa kufuatia shambulio la kombora la Ukraine huko Sevastopol, Crimea, Septemba 13, 2023, katika picha hii ya mitandao ya kijamii.
Meli ya Urusi iliyoharibiwa kufuatia shambulio la kombora la Ukraine huko Sevastopol, Crimea, Septemba 13, 2023, katika picha hii ya mitandao ya kijamii. Crimean Wind via REUTERS - Crimean Wind via Telegram
Matangazo ya kibiashara

"Hakuna shaka hata kidogo kwamba shambulio hilo lilipangwa mapema kwa kutumia uwezo wa kijasusi wa nchi za Magharibi, vifaa vya satelaiti vya NATO, ndege za upelelezi, na kwamba mashambulizi hayo yalitekelezwa kwa ombi la idara za kijasusi za Marekani na Uingereza na kwa uratibu wa karibu na nchi hizo," msemaji wa kidiplomasia wa Urusi Maria Zakharova, ameliambia shirika la habari la AFP.

Crimea - jimbo la Ukraine lililonyakuliwa na Moscow mnamo mwaka 2014 - ndio kitovu cha mfumo wa kijeshi wa Urusi katika mashambulio yake dhidi ya Ukraine, kusambaza wanajeshi wanaoikalia kusini mwa Ukraine na kufanya mashambulizi ya anga. Kyiv, ambayo ilianzisha hivi karibuni mashambulizi kama majibu kwa mashambulizi ya Urusi, inajaribu kuleta mapambano katika eneo hili ambapo imeongeza mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani katika wiki za hivi karibuni. London na Washington hadi sasa hazijajibu shutuma kutoka kwa diplomasia ya Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.