Pata taarifa kuu

Ndege zisizo na rubani 22 za Ukraine zadunguliwa na Urusi karibu na mpaka

Mifumo ya ulinzi wa anga ya Urusi imedungua ndege 19 zisizo na rubani katika Bahari Nyeusi na Crimea na 3 zingine katika majimbo ya Kursk, Belgorod na Orel.

Eneo hilo lililengwa na mashambulizi mapya ya ndege zisizo na rubani wakati wa usiku wa Jumatano hadi Alhamisi. (picha ya kielelezo
Eneo hilo lililengwa na mashambulizi mapya ya ndege zisizo na rubani wakati wa usiku wa Jumatano hadi Alhamisi. (picha ya kielelezo © Anastasiia Smolienko / Avalon / MAXPPP / PHOTOSHOT/MAXPPP
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi mapya kwenye ardhi ya Urusi. Jeshi la Kremlin limedungua ndege 19 zisizo na rubani za Ukraineusiku wa Jumatano Septemba 20 kuamkia Alhamisi Septemba 21 juu ya Bahari Nyeusi na peninsula ya Crimea, pamoja na zingine tatu katika majimbo ya Kursk, Belgorod na Orel, Wizara ya Ulinzi imetangaza leo Alhamisi.

"Mifumo ya ulinzi wa anga iliharibu ndege 19 zisizo na rubani za Ukraine juu ya Bahari Nyeusi na eneo la Jamhuri ya Crimea," wizara imeandika saa nane na dakika 15 kwenye Telegram, na kuongeza kuwa ndege tatu zingine zimedunguliwa katika majimbo ya Kursk, Belgorod (Kusini-Magharibi) na Orel (Magharibi), na kuleta jumla ya idadi ya ndege hadi 22.

Mnamo Agosti 25, chanzo hicho kilidai kwamba Urusi ilidungua ndege 42 za Ukraine huko Crimea, peninsula iliyochukuliwa na Moscow mnamo 2014. Usiku wa Septemba 13 kuamkia 14, Urusi ilisema iliharibu ndege 5 za Ukraine katika Bahari Nyeusi, wakati kikosi cha majini, walipojaribu kushambulia mashua ya doria Sergei Kotov.

Sevastopol yalengwa na mashambulizi siku ya Jumatano

Siku ya Jumatano, mamlaka ilibaini kwamba ilizuia mashambulizi mengine ya Kyiv dhii ya Sevastopol, bandari kubwa kwenye Bahari Nyeusi inayotumiwa na meli za Urusi. Gavana wa Sevastopol Mikhail Razvozhayev amesema kwenye Telegram siku ya Alhamisi kwamba ripoti kwamba ndege zisizo na rubani ziliharibiwa katika eneo la jiji hazikuwa sahihi. "Ndio, ulinzi wa anga unafanya kazi, lakini katika ukanda wa Crimea" unasimamiwa kando na Sevastopol, alihakikisha.

Mashambulio ya Ukraine dhidi ya eneo la Urusi yameongezeka katika miezi ya hivi karibuni dhidi ya hali ya nyuma ya shambulio lililoanzishwa na Kyiv mwanzoni mwa mwezi Juni. Crimea inalengwa mara kwa mara, kama vile majimbo  ya Urusi yanayopakana na Ukraine na Moscow.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.