Pata taarifa kuu

Urusi: Kamanda wa kikosi cha wanamaji wa Urusi aliyetangazwa kuuawa na Kyiv, aonekana

Wizara ya Ulinzi ya Urusi imerusha siku ya Jumanne, Septemba 26, 2023 picha inayoonyesha Viktor Sokolov, kamanda wa kikosi cha wanamaji katika Bahari Nyeusi, akishiriki katika mkutano wa video, ingawa Ukraine inadai kumuua.

Naibu Admirali Viktor Sokolov huko Sevastopol, Septemba 27, 2022.
Naibu Admirali Viktor Sokolov huko Sevastopol, Septemba 27, 2022. REUTERS - ALEXEY PAVLISHAK
Matangazo ya kibiashara

 

Katika picha, afisa huyo anaonekana kwenye skrini kubwa, pamoja na maafisa wengine wakuu wa jeshi wanaohudhuria mkutano ulioongozwa na Waziri wa Ulinzi Sergei Shoigu. Taarifa ambayo haijataja jina la afisa huyo inabaini kwamba mkutano huo ulifanyika siku ya Jumanne. Afisa huyo anaonekana kuwa na mto mkubwa mweupe au kiti cha mkono nyuma ya mgongo wake. Katika video iliyotolewa baadaye, kamanda anaonekana kwenye picha mara kadhaa, bila kuzungumza.

Ukraine siku ya Ijumaa ilishambulia kwa makombora makao makuu ya kikosi cha wanamaji wa Urusi kwenye Bahari Nyeusi huko Sevastopol, mji wa Crimea uliotwaliwa na Urusi. Siku ya Jumatatu, jeshi la Ukraine lilisema kuwa Kamanda Sokolov ni miongoni mwa maafisa thelathini waliouawa katika shambulio hilo la anga.

Lakini, baada ya kurusha hewani kwa picha za Viktor Sokolov, vikosi vya operesheni maalum vya Ukraine vimetangaza siku ya Jumanne kwamba "vinafafanua" habari zao. Vikosi hivi vimethibitisha kwenye Telegram kwamba, kwa mujibu wa "vyanzo vilivyopo", kamanda huyo alikuwa miongoni mwa waliofariki, ingawa utambuzi wa wahasiriwa ulikuwa mgumu kwa sababu miili ilikuwa imeharibika sana. "Kwa kuwa Urusi ililazimika kuchapisha kwa haraka jibu lililodai kuonyesha Sokolov akiwa hai, huduma zetu zinachunguza habari," imesema katika taarifa.

Hakuna mawasiliano ya Urusi juu ya shambulio hilo

Urusi, ambayo karibu kamwe haitoi taarifa juu ya hasara zake za kijeshi, kwa upande wake imetoa tu ripoti ya mtu mmoja kupotea kufuatia shambulio hilo la bomu. Moscow haijatoa maoni yoyote kuhusu madai hayo ya Ukraine, huku Kremlin ikiendelea kusema kuwa haijui siku ya Jumanne kuhusu hatima ya kamanda huyo. "Hakuna habari juu ya suala hili kutoka kwa Wizara ya Ulinzi," Dmitri Peskov, msemaji wa rais wa Urusi, ameambia waandishi wa habari. "Hatuna la kusema," ameongeza, akimaanisha Wizara ya Ulinzi.

Shambulio hilo dhidi ya makao makuu ya kikosi cha wanamaji wa Urusi linaonyesha ugumu unaoongezeka wa Urusi katika kujilinda kutokana na mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani za Ukraine. Walakini, Crimea, peninsula iliyotwaliwa na Urusi mnamo 2014, ni muhimu kwa jeshi la wanamaji la Urusi na vile vile kwa vya wanajeshi wanaoikalia kusini mwa Ukraine. Ukraine, ambayo inaongoza mashambulizi makubwa dhidi ya Urusi na kukomboa maeneo yaliyotwaliwa, inajaribu kugonga upande wa nyuma wa Urusi ili kuvuruga ulinzi na uwezo wa kijeshi.

Baada ya miezi mitatu, hata hivyo, faida ya jimbo hili la Ukraine bado ni ndogo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.