Pata taarifa kuu

Ukraine: Rais Zelensky aithumu Urusi kwa kuwateka watoto

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amehotubia mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, na kuishtumu Urusi kwa kuendeleza vita katika nchi yake na kuwateka watoto, jambo ambalo ameliezea kama mauaji ya kimbari.

Rais Zelensky amezungumzia uvamizi wa Urusi katika mkutano wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York
Rais Zelensky amezungumzia uvamizi wa Urusi katika mkutano wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York AP - Seth Wenig
Matangazo ya kibiashara

Volodymyr Zelensky amekuwa miongoni mwa viongozi  wa kwanza kuzungumza katika mkutano huu maalum, ambapo zaidi ya viongozi sitini wamepangwa kutoa hotuba zao chini ya uenyekiti wa Albania

Rais wa Ukraine ameituhumu Urusi kwa kuwateka watoto
Rais wa Ukraine ameituhumu Urusi kwa kuwateka watoto AP - Seth Wenig

Hii ni mara ya kwanza tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi nchini mwake, Februari 24, 2022, kwa rais Zelensky kuzungumza ana kwa ana mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

“Tunajaribu kuwarejesha nyumbani watoto ila muda inakwenda sana, nini kitatokea? hao watoto walioko kule Urusi wanaichukia Ukraine na uhusiano wowote wa familia zao umevunjika.” amesema rais Zelensky.

Rais wa Marekani Joe Biden, naye pia amelaani vita vinavyoendelea na kuitaka Urusi kusitisha vita.

“Urusi peke yake inawajibika kwenye vita hivi, Urusi pia inauwezo wa kumaliza vita hivi na ndio nchi pake inasimama kinyume na kumaliza vita hivi kwa sababu madai ya Urusi ya amani ni hasara kwa Ukraine.” amesema rais Joe Biden.

Kauli hii inakuja wakati huu viongozi wa dunia wakionekana kugawanyika kuhusu vita vya Urusi nchini Ukraine.

Katika upande mwengine, Rais wa Kenya William Ruto amekutana ana kwa ana na mwenzake wa Ukraine Volodmyr Zelensky pembeni mwa mkutano wa umoja wa mataifa unaondelea jijini New York.

Rais wa Kenya William Ruto amekutana na rais wa Ukraine jijini New York kando ya mkutano wa Umoja wa Mataifa
Rais wa Kenya William Ruto amekutana na rais wa Ukraine jijini New York kando ya mkutano wa Umoja wa Mataifa © Statehouse Kenya

Rais Ruto amesisitiza msimamo wa Nairobi, kutaka kumalizika kwa vita kati ya Ukraine na Urusi.

“Umeonyesha ustahimilivu mkubwa sana nafahamu kwamba haijawa rahisi kwa raia wa Ukraine kuwa imara, tunaunga mkono nilivyosema hapo awali kwamba tunaamini katika mfumo wa ulimwengu unaosimamia sheria.” ameeleza rais William Ruto.

Ukraine imeahidi kujenga ghala la nafaka kwenye bandari ya Mombasa, kusaidia kupambana na uhaba wa chakula kwenye ukanda wa Afrika Mashariki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.