Pata taarifa kuu

Kim Jong Un apokekewa na Waziri wa Ulinzi wa Urusi Vladivostok

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amewasili Vladivostok Mashariki ya Mbali ya Urusi siku ya Jumamosi, ambako amepokeewa na Waziri wa Ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu kabla ya kupanda meli ya kivita, shirika la habari la serikali Tass limetangaza.

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, katikati, akisikiliza maelezo wakati wa ziara yake kwenye kiwanda cha ndege cha Komsomolsk-on-Amur mashariki mwa Urusi, Ijumaa, Septemba 15, 2023.
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, katikati, akisikiliza maelezo wakati wa ziara yake kwenye kiwanda cha ndege cha Komsomolsk-on-Amur mashariki mwa Urusi, Ijumaa, Septemba 15, 2023. AP
Matangazo ya kibiashara

Bw. Kim, ambaye anafanya ziara yake ya kwanza ya kigeni nchini Urusi tangu kuanza kwa janga la UVIKO-19, aliwasili katika uwanja wa ndege wa Knevichi huko Vladivostok kutoka Komsomolsk-on-Amur, ambapo alietembelea viwanda vya ndege siku ya Ijumaa, shirika la habarila serikali Tass imeongeza.

Katika kituo cha anga cha Knevichi, Sergei Shoigu amemuonyesha ndege ya kivita aina ya MiG-31 na mfumo wake wa makombora wa hypersonic Kinjal, kulingana na chanzo hicho.

Siku ya Jumatano, rais wa Urusi Vladimir Putin alitangaza kwamba Kim Jong Un atahudhuria "maonyesho" ya meli za kivita za Urusi huko Vladivostok.

Katika jiji hili kubwa kwenye mipaka ya Urusi, lililo karibu na mpaka wa China na Korea Kaskazini, Kim Jong Un alipanda meli ya kivita ya Urusi Marshal Shaposhnikov, ambapo amepokelewa na kamanda wa meli hiyo.

Pia kamanda mkuu wa kikosi cha wanamaji cha Urusi, Nikolai Yevmenov, ambaye alikuemo katika meli hiyo kubwa, alimweleza kiongozi wa Korea Kaskazini sifa za meli hiyo na silaha zake za kupambana na adui, "mitambo minne ya ya kurusha roketi aina ya RBU -6000," shirika la habari la TASS limeripoti.

Baadaye huko Vladivostok, Bw. Kim pia "atatembelea Chuo Kikuu cha Shirikisho la Mashariki ya Mbali na baadhi ya mitambo ya Chuo cha Sayansi cha Kirusi, ambacho maabara yake yanafanya kazi kwenye biolojia ya baharini," Bw. Putin ameelezea kwa kina katika televisheni ya Urusi.

Rais wa Urusi na kiongozi wa Korea Kaskazini walikutana Jumatano katika uwanja wa ndege wa Vostochny, karibu kilomita 8,000 mashariki mwa Moscow.

Akiwasili nchini Urusi siku ya Jumanne, Bw. Kim alimwalika Bw. Putin kuzuru Korea Kaskazini hivi karibuni, lakini hakuna makubaliano ambayo yametiwa saini kati ya nchi hizo mbili, kulingana na msemaji wa rais wa Urusi Dmitry Peskov.

Nchi za Magharibi zinashuku Moscow kwa kutaka kununua silaha kutoka Pyongyang kwa ajili ya mzozo wa Ukraine. Korea Kaskazini, kwa upande wake, inashukiwa kutaka kupata teknolojia kwa ajili ya mipango yake ya nyuklia na makombora.

- Kubadilishana silaha -

Wakati wa mkutano wao viongozi hao wawili walipeana bunduki, zawadi zinazoonekana kama ishara kutokana na hofu ya nchi za Magharibi.

Wanaume hao wawili walionyesha ukaribu wao, Kim Jong Un akihakikisha kwamba ukaribu na Moscow ulikuwa "kipaumbele kamili" cha sera za kigeni, wakati Bw. Putin alisifu "kuimarishwa" kwa ushirikiano wao.

Rais wa Urusi alitaja hasa "matarajio" ya ushirikiano wa kijeshi licha ya vikwazo vya kimataifa vinavyolenga Pyongyang kwa sababu ya mipango yake ya nyuklia na makombora.

Washington ilikuwa imeeleza "wasiwasi" wake kuhusu uwezekano wa ununuzi wa silaha za Korea Kaskazini, na Seoul "ilikuwa imeonya vikali" dhidi ya shughuli yoyote ya aina hii.

Baada ya kugeukia Iran kuwasilisha mamia ya ndege zisizo na rubani zilizolipuka, Urusi inaweza kupata rasilimali muhimu huko Pyongyang, ambayo ina akiba kubwa ya vifaa vya Soviet na hutengeneza silaha nyingi zilizoafikiwa na wote.Roma and Diana songs - Best music video

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.