Pata taarifa kuu

Urusi yashambulia Bandari muhimu ya Izmail ,Ukraine

Nairobi – Urusi imetumia ndege zake zisizokuwa na rubani kuishambulia upya Ukraine, kwa kuilenga bandari  ya Izmail kwa mara nyingine.Shambulio ambalo limesababaisha moto mkubwa na kuwajeruhi raia 6.

Mwendesha mashtaka wa uhalifu wa kivita anakagua  shambulio la usiku la ndege isiyo na rubani ya Urusi kwenye miundombinu ya karibu ya bandari huko Izmail, Ukraine, Alhamisi, Septemba 7, 2023.
Mwendesha mashtaka wa uhalifu wa kivita anakagua shambulio la usiku la ndege isiyo na rubani ya Urusi kwenye miundombinu ya karibu ya bandari huko Izmail, Ukraine, Alhamisi, Septemba 7, 2023. AP
Matangazo ya kibiashara

Gavana wa eneo la Odesa Oleg Kiper kupitia mtandao wake wa Instagram amesema kuwa Urusi pia imeshambulia kusini  mwa êneo la Odesa.

Urusi imeongeza mashambulio yake katika maeneo  ya Odesa na  Mykolaiv tangu kukwama kwa mradi wa usafirishaji nafaka  kutoka kwa bahari nyeusi.Maaneo hayo yakiwa muhimu kwa usafirishaji wa nafaka za kilimo .

Ukraine ina bandari mbili katika mto Danube, Reni na Izmail. Picha zinazoendelea kuonekana katika mitandao ya kijamii zinaonyesha jinsi Bandari ya Izmail ilivyoshambuliwa.

Kulingana na tarifa ni kuwa wazima moto wapo kwenye êneo hilo kujaribu kuuzima moto na hata kuwaokoa waliojeruhiwa.Kufikia sasa watu zaidi ya sita wameripotiwa kufikishwa hospital.

Hapo awali, Kiper alikuwa amewataka watu katika wilaya ya Izmail kusalia katika eneo salama hadi arifa za uvamizi wa anga zitakapokoma.

Izmail, katika mpaka na Romania mwanachama wa NATO, imekuwa njia kuu ya usafirishaji wa bidhaa za Ukraine kufuatia Urusi kujiondoa katika mkataba wa nafaka uliosimamiwa na Umoja wa Mataifa mwezi Julai.

kwa upande mwingine Jeshi la Ukraine limesema kwamba limekomboa vinu vya mafuta na gesi kwenye bahari ya Black Sea kutoka mikononi mwa Urusi likieleza hatua hiyo kuwa muhimu katika kuchukua tena udhibiti wa Crimea.

Ripoti zinaongeza kuwa wapiganaji wa Ukraine wamepiga hatua kubwa kuelekea kukomboa Bakhmut, mji uliyozingirwa baada ya kuchukuliwa na Russia hapo Mei. Kwa kukomboa vinu hivyo Kyiv imepata nguvu zaidi kwenye vita vyake dhidi ya Russia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.