Pata taarifa kuu

Ukraine: Ukraine yadai kudungua ndege zisizo na rubani juu ya anga ya mji mkuu

Mfumo wa ulinzi wa anga wa Ukraine wameangusha zaidi ya ndege 20 zisizo na rubani za Urusi zilizokuwa zikilenga mji mkuu wa Ukraine, Kiev siku ya Jumapili alfajiri, imetangaza mamlaka nchini Ukraine, ambayo imeripoti mtu mmoja kujeruhiwa na vifusi vilivyoanguka.

Picha hii iliyopigwa na kutolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ukraine mnamo Septemba 6, 2023 inaonyesha maafisa wa polisi wa Ukraine wakiwa kwenye eneo lililolengwa namashambulizi ya Urusi huko Kostyantynivka,katika jimbo la Donetsk, mashariki mwa Ukraine. Rais wa Ukraine alisema mashambulizi haya ya Urusi katika soko la mashariki mwa Ukraine yaliua zaidi ya watu kumi na kujeruhi wengine wengi wakati waziri wa mambo ya nje wa Marekani alipozuru Kyiv.
Picha hii iliyopigwa na kutolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ukraine mnamo Septemba 6, 2023 inaonyesha maafisa wa polisi wa Ukraine wakiwa kwenye eneo lililolengwa namashambulizi ya Urusi huko Kostyantynivka,katika jimbo la Donetsk, mashariki mwa Ukraine. Rais wa Ukraine alisema mashambulizi haya ya Urusi katika soko la mashariki mwa Ukraine yaliua zaidi ya watu kumi na kujeruhi wengine wengi wakati waziri wa mambo ya nje wa Marekani alipozuru Kyiv. AFP - HANDOUT
Matangazo ya kibiashara

Kwa sasa kumekuwa na vita vya maneno kati ya nchi hizi mbili hasimu. Kila nchi imekuwa ikidai kuangusha ndege za upande mwingine bila hata hivyo kutoa ushahidi tosha.

Vita vya Urusi nchini Ukraine sasa vimedumu zaidi ya mwaka mmoja, tangu mwezi Februari, tarehe 24 mwaka 2022.

Hata hivyo nchi zote mbili zinaendelea kupoteza katika vita hii visiokoma, huku kila upande ukiwa na washirika wanaousaidia katika vita hivi.

Majaribio ya kusitishwa kwa vita hivyo yamegonga mwamba mara kadhaa, huku baadhi ya nchi zikidai kujaribu kusuluhisha mgogoro huo bila mafaanikio.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.