Pata taarifa kuu

China:Tamko la pamoja la viongozi wa G20 mjini Delhi ni Ishara nzuri

Nchi zenye uchumi mkubwa zaidi duniani zilipitisha rasmi tamko hilo la pamoja katika mkutano wa G20 nchini India, bila hata nukta moja pinzani, siku ya Jumapili.

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi,akisalimiana na Waziri Mkuu wa China Li Qiang alipowasili katika kituo cha Bharat Mandapam kwa ajili ya Mkutano wa G20 mjini New Delhi, India,
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi,akisalimiana na Waziri Mkuu wa China Li Qiang alipowasili katika kituo cha Bharat Mandapam kwa ajili ya Mkutano wa G20 mjini New Delhi, India, AP - Evan Vucci
Matangazo ya kibiashara

China imesema taarifa hiyo inaakisi maoni yake na kuonyesha kuwa  mataifa ya G20 yanafanya kazi pamoja ili kukabiliana na changamoto za kimataifa na kukuza maendeleo.

Hii ni mara ya kwanza kwa Beijing kutoa maoni yake kuhusu tamko hilo.

Nchi nyingine kadhaa, ikiwa ni pamoja na Uingereza na Marekani, zimepongeza taarifa hiyo ya pamoja, ambayo inaepuka kulaani Urusi, mshirika mkuu wa kimkakati wa China, kwa vita vyake dhidi ya Ukraine. Urusi pia imepongeza tamko hilo kama "hatua muhimu". Lakini Ukraine, ambayo haikuwakilishwa katika mkutano huo, imeelezea kusikitishwa kwake ikisema kuwa tamko hilo "hakuna la kujivunia".

Ujumbe wa China kwenye mkutano huo uliongozwa na Waziri Mkuu Li Qiang baada ya Rais Xi Jinping kukosekana. Uhusiano kati ya China na India bado haujazimika kutokana na mzozo wa mpaka uliosababisha mapigano miaka mitatu iliyopita ambapo wanajeshi 20 wa India na wanne wa China waliuawa.

Katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumatatu, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Mao Ning alisema kuwa China daima imekuwa ikiunga mkono G20 na inaamini kwamba wanachama wake wanapaswa "kusimama kwa mshikamano na kushirikiana katika masuala ya kimataifa".

Alikuwa akijibu swali la Huduma ya Habari ya China kuhusu maoni ya Beijing kuhusu mkutano huo na matokeo yake.

"Mkutano huo ulipitisha tamko la viongozi, ambalo linaonyesha pendekezo la China na kusema kwamba G20 itachukua hatua madhubuti kupitia ushirikiano, na kutoa ishara chanya ya G20 kufanya kazi kwa pamoja ili kukabiliana na changamoto za kimataifa na kukuza ufufuaji wa uchumi wa dunia na maendeleo ya kimataifa," Bi. Ning alisema.

Aliongeza kuwa China ilichukua jukumu la kujenga na "kuunga mkono mkutano huo katika kutilia maanani wasiwasi wa nchi zinazoendelea" ili kufikia "matokeo yenye matunda".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.