Pata taarifa kuu

Ukraine: Takriban raia 17 wauawa katika shambulizi la anga la Urusi kwenye soko la mashariki

Kwa mujibu wa rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, shambulio la anga katika soko la mashariki mwa nchi hiyo, karibu na Bakhmut, yaliua takriban watu 16 Jumatano hii.

Picha hii iliyopigwa na kutolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ukraine mnamo Septemba 6, 2023 inaonyesha polisi wa Ukraine wakiwa kwenye eneo la shambulio la Urusi huko Kostyantynivka, katika jimbo la Donetsk, mashariki mwa Ukraine.
Picha hii iliyopigwa na kutolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ukraine mnamo Septemba 6, 2023 inaonyesha polisi wa Ukraine wakiwa kwenye eneo la shambulio la Urusi huko Kostyantynivka, katika jimbo la Donetsk, mashariki mwa Ukraine. AFP - HANDOUT
Matangazo ya kibiashara

"kikosi cha kigaidi cha nchi kavu cha Urusi kimeua watu 16 katika mji wa Kostiantynivka, mkoa wa Donetsk," Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameandika kwenye mtandao wa kijamii. Kulingana rais wa Ukraine, ni soko na maduka ambayo yaliathirika. Kwa hivyo ameonya kwamba "kwa bahati mbaya, idadi ya vifo na majeruhi inaweza kuongezeka". Shambulio hilo lilipiga mji huo saa nane na dakika 4 mchana , anaripoti mwandishi wetu wa Ukraine, Pierre Alonso.

Watu wengine 31 wamejeruhiwa katika shambulio hili la Urusi ambalo lilipiga mji huo karibu na Bakhmut, eneo la vita vya umwagaji damu inayoendeshwa na wanajeshi wa Moscow kwa zaidi ya mwaka mmoja, mashariki mwa nchi hiyo. "Operesheni ya uokoaji inaendelea. Bado kuna watu wako chini ya vifusi," imeongeza ofisi ya mashtaka kwenye Telegram.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock amelaani shmbulio hilo siku ya Jumatano. "Shambulio hili la kikatili kwa watu wasio na hatia wakifanya shughuli zao za biashara kwa amani sokoni linaonyesha wazi kwamba vita vya uvamizi vya Urusi ni shambulio dhidi ya sheria za kimataifa na binadamu," Baerbock ameandika kwenye X (zamani ikiitwa Twitter).

Mapema Jumatano hii, shambulio la ndege zisizo na rubani za Urusi lilisababisha kifo cha mtu mmoja katika eneo la Odessa, kusini, ambapo miundombinu ya bandari muhimu kwa mauzo ya nafaka inalengwa mara kwa mara. Tangu kuanza kwa mzozo nchini Ukraine, Urusi imedai kulenga maeno ya kijeshi pekee.

Shambulio hili linakuja wakati Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alipofanya ziara ya kushtukiza siku ya Jumatano. Wakati wa mkutano wake na Rais Zelensky, alisisitiza uungaji mkono wa Washington kwa Kyiv katika mapambano yake ya ukombozi wa maeneo ya kusini na mashariki. "Rais (Joe) Biden aliniomba nije na kuthibitisha kwa nguvu uungwaji mkono wetu," alisema, akibainisha kwamba "maendeleo makubwa yaliyopatikana mashambulizi yao kujibu mashambulizi ya Urudi" yalikuwa "ya kutia moyo."

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.