Pata taarifa kuu

Urusi yadai kuangusha ndege tatu zisizo na rubani Magharibi

Ulinzi wa Urusi umedungua ndege tatu zisizo na rubani katika mikoa ya magharibi ya Moscow, Kaluga na Tver, mamlaka imetangaza Jumanne asubuhi. 

Wizara ya Ulinzi ya Urusi imedai kwamba imedungua ndege 3 zisizo na rubani.
Wizara ya Ulinzi ya Urusi imedai kwamba imedungua ndege 3 zisizo na rubani. © Alexander Nemenov, AFP
Matangazo ya kibiashara

 

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un anapanga kuzuru Urusi mwezi huu kukutana na rais wa Urusi Vladimir Putin na kujadiliana naye uwezekano wa Pyongyang kuipa Moscow silaha.

Wakati huo huo serikali ya Cuba ilisema siku ya Jumatatu kuwa imetambua "mtandao haramu" wa Urusi unaolenga kuwaajiri Wacuba kwa "operesheni za kijeshi nchini Ukraine" na imeanzisha kesi za uhalifu dhidi ya waliohusika.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Cuba "inafanya kazi ya kupunguza na kusambaratisha mtandao wa biashara haramu ya binadamu unaofanya kazi kutoka Urusi ili kuwajumuisha raia wa Cuba wanaoishi huko, na hata wengine kutoka Cuba, katika vikosi vya kijeshi vinavyohusika katika operesheni za kijeshi nchini Ukraine," Wizara ya Mambo ya Nje ilisema katika taarifa.

Waziri wa Mambo ya Nje, Bruno Rodriguez, amehakikishia, katika ujumbe uliochapishwa kwenye X (zamani ikiitwa Twitter), kwamba serikali ya Cuba "inatumia sheria" dhidi ya operesheni hizi. Wizara imesema ilikuwa imeanzisha "mashitaka ya jinai dhidi ya waliohusika katika shughuli hizi", bila kutoa maelezo. Amebaini kwamba Cuba haishiriki katika vita vya Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.