Pata taarifa kuu

Wanajeshi sita wafariki katika ajali ya helikopta mbili za kivita mashariki mwa Ukraine

Wanajeshi sita wa Ukraine wamefariki katika ajali ya helikopta mbili za kivita mashariki mwa Ukraine, ambapo jeshi la Kiev linaongoza mashambulizi dhidi ya vikosi vya Urusi, Ofisi ya taifa ya Upelelezi ya Ukraine (SBI) imetangaza Alhamisi.

Ndege za kivita za Ukraine za Su-27 zinaruka katika eneo la Zhytomyr nchini Ukraine, Desemba 6, 2018.
Ndege za kivita za Ukraine za Su-27 zinaruka katika eneo la Zhytomyr nchini Ukraine, Desemba 6, 2018. © Mikhail Palinchak/AP
Matangazo ya kibiashara

"Helikopta mbili za kijeshi za Mi-8 zimeanguka wakati wa misheni ya vita. Wanajeshi sita wa jeshi la Ukraine wamefariki,” imesema taarifa kutoka SBI, ikibainisha kuwa ajali hiyo ilitokea siku ya Jumanne katika eneo la Kramatorsk.

Wakati huo Urusi imedai kuharibu ndege isiyo na rubani ya Ukraine leo Alhamisi Agosti 31 katika mkoa wa Moscow, shambulio ambalo halikusababisha hasara kwa mujibu wa meya wa mji mkuu.

Alhamisi asubuhi, ndege isiyo na rubani "iliharibiwa na (...) mfumo wa ulinzi wa anga katika eneo la wilaya ya Voskresensky katika mkoa wa Moscow", kusini mashariki mwa mji mkuu, imesema Wizara ya Ulinzi ya Urusi kwenye Telegram, ambayo imeshutumu Kyiv kwa kutekeleza shambulio hilo. Kulingana na meya wa Moscow, Sergei Sobyanin, ndege hiyo "ilikuwa ikiruka kuelekea Moscow", ameonyesha kwenye mtandao huo wa kijamii.

Mashambulizi ya ndege zisizo na rubani dhidi ya Urusi na peninsula ya Crimea iliyotwaliwa yamekuwa yanafanyika kila siku katika wiki za hivi karibuni, hasa yakilenga mji mkuu wa Urusi, katikati mwa mashambulizi yaKiev  yaliyoanza mapema mwezi Juni. Shambulio la ndege isiyo na rubani liliharibu au kuharibu ndege kadhaa za kijeshi kwenye uwanja wa ndege wa Pskov kaskazini magharibi mwa Urusi, siku ya Jumatano,ikiwa ni jambo la nadra. Jeshi la Urusi pia limebaini kwamba liliangamiza ndege nyingi katika mikoa ya magharibi ya Moscow, Bryansk, Orel, Kaluga na Ryazan, na pia katika Crimea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.