Pata taarifa kuu

Urusi yadai kuharibu boti nne za kikosi maalum cha Ukraine katika Bahari Nyeusi

Urusi imedai mapema Jumatano kwamba imeharibu boti nne za mwendo kasi katika Bahari Nyeusi ambazo zilibeba jumla ya hadi wanajeshi 50 wa kikosi maalum cha Kyiv ambacho mamlaka ya Urusi imesema kilifanya mashambulizi kadhaa ya usiku kwa ndege zisizo na rubani katika ardhi ya Urusi.

Kikosi cha wanajeshi wa Urusi.
Kikosi cha wanajeshi wa Urusi. © Russian Army
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatano karibu saa sita usiku saa za Urusi, "ndege ya Jeshi la Wanamaji la Kikosi cha Bahari Nyeusi (...) imeharibu botii nne za kijeshi za mwendo kasi (ambazo zilikuwa zimebeba) makundi ya wanajeshi 50 wa vikosi maalum vya Ukraine", wizara ya ulinzi imesema kwenye Telegram bila kutoa taarifa zaidi.

Wakati wa usiku, mfumo wa ulinzi wa anga pia ulifanya kazi ya kurudisha nyuma "mashambulizi ya ndege zisizo na rubani ya adui (yaliyokuja) kutoka baharini" kwenye eneo la ghuba ya Sevastopol, makao makuu ya meli za Urusi katika Bahari Nyeusi iliyoanzishwa huko Crimea, amesema Gavana wa Urusi Mikhail Razvojayev, kabla ya kueleza kuwa hali hiyo "imedhibitiwa".

"Vikosi (vya kuzuia dhidi ya hujuma za manowari) vimemaliza kazi yao katika eneo la baharini. Kwa sasa, hakuna taarifa sahihi kuhusu idadi na aina ya malengo yaliyoharibiwa," amesema Bw. Razvojayev kwenye Telegram.

Ukraine ilijipongeza siku ya Alhamisi kwa kutekeleza operesheni adimu ya kikomandoo katika rasi ya Crimea, iliyotwaliwa na Moscow mwaka 2014, na kwa kupandisha bendera ya taifa huko, mafanikio ya kiishara katika ngome hii inayofikiriwa kuwa haiwezi kuzuilika na Moscow.

Vikosi vya vikosi maalum vya Ukraine vilikuwa vimetoka baharini, vikitua magharibi mwa Crimea, kabla ya kuondoka "bila hasara" kulingana na ujasusi wa kijeshi wa Ukraine.

Mnamo Agosti 22, Urusi pia ilidai "iliharibu" boti lililokuwa limebeba wanajeshi wa Ukraine karibu na Kisiwa cha Serpents, katika Bahari Nyeusi, baada ya kudai siku hiyo hiyo kuwa ilikuwa meli iliyokuwa ikifanya upelelezi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.