Pata taarifa kuu

Urusi: Kikomo cha umri kwa askari wa akiba chaongezwa kwa miaka mingine mitano

Nchini Urusi, kikomo cha umri cha askari wa akiba kimeongezwa kwa miaka mitano. Vladimir Putin leo amethibitisha mabadiliko katika sheria ambayo itaanza kutumika Januari 1. Mageuzi ambayo, kulingana na wabunge waliounga mkono mradi huo, yataboresha ulinzi wa nchi

Askari wa akiba wa Urusi wakati wa mafunzo katika mkoa wa Donetsk mnamo Oktoba 4, 2022.
Askari wa akiba wa Urusi wakati wa mafunzo katika mkoa wa Donetsk mnamo Oktoba 4, 2022. REUTERS - ALEXANDER ERMOCHENKO
Matangazo ya kibiashara

'Umri wa juu kwa aina zote za askari wa akiba wa jeshi la Urusi umeongezwa kwa miaka mitano. Askari, mabaharia na sajenti wanaweza kuhudumu hadi umri wa miaka 55. Umri huu utakuwa miaka 60 kwa maafisa, yaani hadi cheo cha nahodha, 65 kwa maafisa wakuu na 70 kwa majenerali. Hata hivyo, marekebisho bado yanawezekana kwa watu wanaohusika katika kipindi cha mpito ambacho kitaendelea hadi mwaka 2028.

Wakati wa kupitishwa kwa muswada huu na mabunge, mbunge mmoja amesema kuwa marekebisho haya yanakusudiwa kuboresha usalama wa Shirikisho la Urusi na kuboresha uwezo wa ulinzi wa nchi. Ukweli unabaki kuwa marekebisho haya yalipendekezwa mnamo Novemba 2022, ambayo ni kusema baada ya tangazo la kurejeshwa kwa askari wa akiba 300,000 ndani ya mfumo wa shughuli nchini Ukraine. Uhamasishaji wa sehemu ambao ulikuwa umesababisha mamia ya maelfu ya askari wenye umri wa kupigana kukimbilia nje ya nchi.

Kwa vifungu hivi vipya, jeshi la Urusi litakuwa na idadi ya ziada ya wapiganaji wapya, ambayo inaweza kuliwezesha kuepuka kutafuta msaada, kwa hatua ya kwanza, kwa uhamasishaji wa jumla, ikiwa hilo litahitajika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.