Pata taarifa kuu
ULINZI-DIPLOMASIA

Rais wa Belarus anajadili nia ya Wagner ya kufanya operesheni nchini Poland

Rais wa Belarus amewasili Saint Petersburg kukutana kwa mazungumzo na Vladimir Putin. Wawili hao wamejadili mgogoro wa Ukraine na hali ya wapiganaji wa kundi la Wagner huko Belarus ambao, kulingana na Alexander Lukashenko wana hasira ya kupindukia na wanapenda kwenda Warsaw kufanya operesheni.

Rais wa Urusi Vladimir Putin na rais wa Belarus Alexander Lukashenko huko Kronstadt, karibu na mji wa Saint Petersburg, Julai 23, 2023.
Rais wa Urusi Vladimir Putin na rais wa Belarus Alexander Lukashenko huko Kronstadt, karibu na mji wa Saint Petersburg, Julai 23, 2023. AP - Alexander Demianchuk
Matangazo ya kibiashara

Mkutano kati ya Vladimir Putin na Alexander Lukasjenko, mshirika mkubwa wa Kremlin, unakuja karibu mwezi mmoja baada ya uasi wa Wagner nchini Urusi, ambapo kiongozi wa Belarus alichukua jukumu la kusitishwa kwa uasi huo. Ishara ya umuhimu wa mazungumzo haya ya kwanza ya ana kwa ana tangu kipindi hiki kigumu kwa Kremlin ambacho kilitikisa mamlaka ya Urusi, Vladimir Putin alisema siku ya Jumapili kwamba viongozi hao wawili "watafanya siku moja na nusu au siku mbili" kwa mazungumzo haya ya nchi mbili.

Β  Katika mpango huo, tutajikita hasa na "usalama katika eneo letu", alithibitisha rais wa Urusi, katika maelezo ya awali yaliyotangazwa kwenye runinga ya Urusi. Valdimir Putin na Alexander Lukashenko pia watalazimika kujadili faili muhimu la kundi la wanamgambo Wagner, ambalo kiongozi wake, Yevgeny Prigozhin, alidai kutaka kupindua uongozi wa kijeshi wa Urusi. Kulingana na Kremlin na kile anachosema mwenyewe, Alexander Lukashenko allikuwa kama mpatanishi kati ya ikulu ya Kremlin na Yevgeny Prigozhin kutafuta suluhisho la haraka kwa uasi huo.

'Wanaume wa Wagner wanaomba kwenda magharibi'

Katika makubaliano yaliyofikiwa kati ya pande hizo, ilipendekezwa kwa wapiganaji wa Wagner kusaini mkataba na jeshi la serikali ya Urusi, kujiunga na maisha ya kiraia au sivyo kwenda Belarus. Tangu wakati huo, baadhi ya wapiganaji wa kundi hili ambao wamepata uzoefu wa mapigano wako katika nchi hii jirani ya Urusi. Alexander Lukashenko hivyo alihakikisha Jumapili mbele ya Vladimir Putin kwamba "anawahifadhi" wapiganaji wa Wagner katikati mwa Belarus, akidai "kudhibiti" hali ya mambo. β€œWameanza kutuchosha. Wanaomba "kwenda magharibi" (…) kwenda Warsaw, RzeszΓ³w", Alexander LukaszΓ³w awali alitangaza kwa mwenzake wa Urusi, ambaye alionekana akitabasamu kidogo. "Lakini, kwa kweli, ninawahifadhi katikati mwa Belarus, kama tulivyokubaliana," aliongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.