Pata taarifa kuu

Ukraine: Urusi yaonya shehena yoyote ya nafaka katika Bahari Nyeusi

Katika Bahari Nyeusi, vita vinajidhihirisha tena. Baada ya mwaka mmoja kusitishwa kwa mapigano kwa sababu ya makubaliano ya usafirishaji wa bidhaa za kilimo, Moscow imetangaza kwamba meli yoyote itakayopatikana ikitembea katika Bahari Nyeusi itachukuliwa kuwa meli ya kivita. Tangazo hilo limetolewa siku ya Jumatano, Julai 19, siku moja baada ya kusahmbuliwa kwa bandari ya Odessa nchini Ukraine.

Meli ya shehena ya nafaka 'TQ Samsun', ilitia nanga katika Bahari Nyeusi karibu na Mlango wa Bahari wa Bosphorus huko Istanbul, Uturuki, Jumatatu, Julai 17, 2023.
Meli ya shehena ya nafaka 'TQ Samsun', ilitia nanga katika Bahari Nyeusi karibu na Mlango wa Bahari wa Bosphorus huko Istanbul, Uturuki, Jumatatu, Julai 17, 2023. AP - Sercan Ozkurnazli
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Moscow, Jean-Didier Revoin

Baada ya mashambulio yaliyolenga bandari ya Odessa, yakiharibu maghala ya nafaka, Moscow inachukulia, tangu Jumatano, meli yoyote inayoelekea bandari ya Ukraine kwenye Bahari Nyeusi kama ya kijeshi, bila kujali bendera yake.

Hizi ni athari ya kutorejeshwa upya kwa makubaliano ya mauzo ya nafaka ya Ukraine ambayo yanahitimisha njia zisizohamishika za kijeshi zilizoanzishwa mwaka mmoja uliopita. Hali hii inarejea kama hapo, hali ambayo Vladimir Putin anaihusisha na nchi za Magharibi.

Kwa sababu machoni pake, Moscow imeonyesha subira ya kupindukia kwa kuyafanya upya makubaliano hayo mara kadhaa kwa matumaini ya kuona nchi za Magharibi zikitekeleza vifungu vilivyoihusu Urusi.

Rais wa Urusi amesisitiza kwamba sasa anasubiri hatua madhubuti juu ya matumizi ya vifungu vyote vinavyohusu Urusi ili kuanza tena mazungumzo na sio ahadi mpya.

Ameongeza pia kuwa Moscow ilikuwa tayari kuchukua nafasi ya wingi wa nafaka za Ukraine zinazouzwa nje, na hata kuzipatia nchi maskini bila malipo. Njia ya kuwaweka Wamagharibi mbele ya majukumu yao kwa kujisafisha wenyewe kutokana na dhima yoyote ya kuzorota kwa hali ya Bahari Nyeusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.