Pata taarifa kuu
Iran-Umoja wa Ulaya

Serikali ya Iran kumaliza mazungumzo na nchi zenye nguvu duniani juu ya mpango wake wa Nyuklia

Mataifa yenye nguvu duniani pamoja na Iran, yamerejea kwenye mazungumzo jijini Vienna juu ya kutafuta suluhu ya kudumu kuhusu mzozo wa Nyuklia wa Iran. Hii ni mara ya tatu mfululizo pande hizi mbili zinakutana kwa ajili ya mazungumzo tangu pale serikali ya Teheran ilipokubali kuchumguzwa kwa vinu vyake vya Nyuklia Novemba iliopita

Catherine Ashton na waziri wa mambo ya nje wa Iran Minister Mohammad Javad Zarif jijini Vienna
Catherine Ashton na waziri wa mambo ya nje wa Iran Minister Mohammad Javad Zarif jijini Vienna Reuters/Heinz-Peter Bader
Matangazo ya kibiashara

Mohammad Javad Zarif, waziri wa mambo ya nje wa Iran pamoja na mkuu wa sera za mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya bi Catherine Ashton, ambaye anaongoza ujumbe wa nchi sita ikiwa ni pamoja na Ujerumani, China, Marekani Uingereza, Ufaransa na Urusi, wamezinduwa majadiliano yenye kuwa na matumaini ya kutowa mwanga zaidi kuhusu mpango wenye utata wa Nyuklia wa Iran.

Pande hizo mbili katika mazungumzo zinampango wa kuharakisha mazungumzo hayo ili kufikia mwezi Mei mwaka huu waanza kuandika nakala za mwisho kuhusu mazungumzo hayo. Wataalamu wa maswala ya sheria kutoka nchini Iran tayari wamejiunga wa serikali jijini Vienna kwa lengo kuongexza chachu katika mazungumzo hayo.

Makubaliano yanayo tarajiwa yatapelekea kufutwa kwa vikwazo vyote vilivyowekewa na mataifa hayo yenye nguvu kwa serikali ya Teheran, iwapo tu itadhihirika wazi kwamba Iran haina mpango wowote wa kutengeneza bomu za Atomiki.

Kwa sasa muafaka unatakiwa kupatikana juu ya mtazamo wa Iran ambayo inajitetea kuwa na haki ya kuwa na mapngo wa Nyuklia, ambapo mataifa ya magharibi yamekuwa yakiushukia kuwa na mpango wa kutengeneza bomu za nykulia.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.